DRC : Viongozi wa dini kukutana na wanasiasa kutafuta suluhu ya mzozo

Nchini DRC, ujumbe wa Kanisa Katoliki na Kanisa la Protestante, madhehebu mawili makuu ya kidini nchini humo, unaendelea na mashauriano yake ikiwa ni sehemu ya mpango wao unaoitwa “mkataba wa kijamii wa amani na kuishi pamoja vizuri katika DRC na eneo la Maziwa Makuu.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kukutana na Mratibu wa AFC/M23 Mjini Goma ujumbe huo uliekea mjini Kigali nchini Rwanda, kukutana na Rais wa Rwanda Paul Kagame, kama sehemu ya mkutano wao mashauriano ya “Mkataba wa Kijamii kwa ajili ya amani na kuishi vizuri pamoja nchini DRC.”

Na sasa ujumbe huo umepanga kwenda Ulaya mwanzoni mwa juma lijalo ambako wamepanga kukutana na viongozi mbalimbali wa kisiasa akiwemo Moise Katumbi katika muendelezo wa mazungumzo ambayo tayari walianzisha jijini Kinshasa baada ya kukutana na Martin Fayulu na Denis Sesanga.

Wamepanga pia kukutana na wajumbe wa rais Joseph Kabila alietuhumiwa kuwa nyuma ya AFC/M23, wajumbe mbalimbali wapinzani wa rais Felix Tshisekedi nao wamepangwa kukutana na wajumbe hao wakiongoezwa na Mbunge Andre Lubaya. Itakuwa fursa kujadili kwa kina kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini DRC na swala la kuachiwa huru wafungwa wa kisiasa akiwemo Seth Kikuni.

Wajumbe hao wamepanga pia kukutana na viongozi kadhaa wa bara la Afrika katika siku zijazo na baadae watarejea jijini Kinshasa kufanya tathmini na kupanga mikakati ya hatuwa itayofuata.