DRC: Usimamizi wa wakimbizi wa ndani umekuwa mgumu zaidi tangu M23 kudhbiti Goma

Usimamizi wa wakimbizi wa ndani nchini DRC unazidi kuwa mgumu. Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya kibinadamu pamoja na kuratibu masuala ya dharura OCHA, karibu watu 700,000 wamekimbia tangu mwka 2023. 

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwisho wa mwezi wa Januari, M23, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda, wamewasili katika maeneo mapya, ikiwa ni pamoja na Goma na Bukavu, na kusababisha wakimbizi wapya ndani. Misaada ya kibinadamu, ambayo tayari iko chini ya shinikizo, inajitahidi kuendana na ukubwa wa mgogoro. Wito unaongezeka wa kufunguliwa kwa eneo salama kwa watu.

Idadi kubwa ya watu wanaoooka makazi yao kutokana na machafuko ya hivi karibuni nchini DRC inazidi kuongezeka siku baada ya siku, kulingana na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA).

Kabla ya kuwasili kwa M23, wakiungwa mkono na Rwanda, maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kutoka maeneo ya Masisi, Lubero na Rutshuru walikuwa wamepata hifadhi huko Goma na Minova, maeneo mawili ambapo makumi ya maelfu ya watu walikuwa walikusayika.

Lakini kuvunjwa kwa kambi hizo baada ya makataa ya M23 mnamo Februari 9 kulazimisha watu wengi waliokimbia makazi yao kurejea katika maeneo ambayo hayana tena miundombinu yoyote ya kimsingi. Kurudi kwa lazima, wakati mashirika ya kutoa misada ya kibinadamu yenyewe yanashinwa kukabiliana na dharura, kutokana na ukosefu wa rasilimali kufuatia mapigano ya hivi karibuni.

Eujin Byun, msemaji wa UNHCR, anaonya kuhusu hali hiyo: “Tuna wasiwasi na vifaa nchini, kwani maghala mengi ya mashrika ya kutoa misaada ya kibinadamu yaliporwa wakati wa vita. Kila kitu ambacho watu hawa wanahitaji lazima kipitie kwenye eneo salama lililotengwa, yaani, uwanja wa ndege na bandari. Hata hivyo, upatikanaji wa miundombinu hii kwa sasa ni mdogo sana. Mara tu tunaweza kufikia watu waliolazimika kutoroka makazi yao, tutahitaji kabisa vifaa hivi kuingia mashariki mwa Kongo ili kuwasaidia. “

Hali ni tete, na watu wanaendelea kukimbia mapigano. Huko Kivu Kaskazini, mapigano yanasaabisha maelfu ya watu waliokimbia makazi yao kukimbia tena. Lakini wengi hawana pa kwenda: 60 hadi 70% ya kambi zimeharibiwa. Wamekwenda wapi? Vigumu kusema. Huenda wengine wamekumbilia mji jirani, wengine bado wako Goma. Tunachojua ni kwamba watu waliotoroka makazi yao wanapata hifadhi katika hospitali, shule zilizo tupu, majengo yaliyotelekezwa. Wengi pia wanalala barabarani. Lakini kwa wale wote wasioweza kufikiwa, haiwezekani kuwa na makadirio. Katika mkoa wa Kivu Kusini, hali ni kama hiyo. Mzozo huo unaenea, unasukuma watu kuelekea Bukavu, na wengine wanavuka mpaka na kuingia Burundi. Lakini kwa sababu ya ukosefu wa ufikiaji, haiwezekani kukadiria idadi yao halisi. Ikiwa mapigano yataendelea mashariki mwa nchi, idadi hii itakuwa kubwa zaidi.

Kulingana na OCHA, karibu watu 300,000 walikimbia katika wiki za hivi karibuni, idadi ambayo inaweza kuongezeka zaidi ikiwa mapigano yataendelea.