
Wakati mzozo wa kibinadamu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ukizidi kuwa mbaya kufuatia mashambulizi mapya ya waasi wa M23, Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Watoto, UNICEF, lina hofu kutokana na kukithiri kwa ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kuibuka tena kwa vita katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC, kumewalazimu zaidi ya watu 850,000, karibu nusu yao wakiwa watoto, kukimbia.
Wengi wao wanaishi katika mazingira hatarishi, wakipewa hifadhi mashuleni, makanisani na wengine kulala nje usiku, wakiwa na uwezo mdogo wa kupata maji safi, usafi wa mazingira, huduma za afya na elimu.
Ghasia zinazoendelea katika mkoa huo zimesababisha ongezeko kubwa la ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto.
Kesi zilizothibitishwa zimeongezeka sana tangu mwezi wa Januari 2025, ongezeko la takriban 150% ikilinganishwa na mwezi wa Desemba 2024.
Ukiukaji huu ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, mauaji, ukeketaji, na watoto kulazimishwa kujiunga katika makundi yenye silaha na matumizi ya watoto na makundi yenye silaha.
Hivi karibuni Mwakilishi wa UNICEF nchini DRC alitembelea eneo la mashariki mwanzoni mwa mwezi Machi ili kujionea athari za mgogoro wa Bukavu na kutathmini majibu makubwa ya UNICEF.