DRC: Uhaba wa fedha wasababisha wakazi wa Goma kwenda Rwanda

Sasa imepita zaidi ya mwezi mmoja tangu kundi la waasi la M23 – linaloungwa mkono na Rwanda – kuiteka Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Na, kwa zaidi ya mwezi mmoja, taasisi za kifedha za jiji zimebaki zimefungwa. Wakikabiliwa na tatizo la ukosefu wa upatikanaji wa fedha, wakazi wanatafuta na kupata suluhu mbadala, ikiwa ni pamoja na kuvuka mpaka mji mji pacha wa Gisenyi nchini Rwanda.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Lucie Mouillaud

Katika maegesho ya benki moja huko Gisenyi, karibu magari yote yaliyoegeshwa yamesajiliwa DRC. Eddy de Paul, mkazi wa Goma, amevuka mpaka wa Great Barrier (Grande Barrière) asubuhi: “Tangu vita vya M23, mashambulizi ya M23 katika mji wa Goma, hii ni mara ya tatu nimekuja Rwanda kuchukua pesa, kwa sababu lazima nilipe bili, familia inatakiwa kuishi. “

Hali mbaya ya kiuchumi

Kila siku, kutokana na ukosefu wa ukwasi huko Goma, wakazi wengi huenda Gisenyi kuchukua pesa, kutoka kwa akaunti zao za benki au kutoka ofisi za Western Union: “Benki hazifanyi kazi,” Eddy anasema, “wala ATM hazifanyi kazi. Watu hata hawajui jinsi ya kuishi tena. Hali ya uchumi imekuwa mbaya sana. Kwa sasa, hatuoni matarajio yoyote ya siku zijazo na uboreshaji wa hali hiyo, kwa sababu hakuna kitu cha kutia moyo. “

“Ni ngumu”

Akiandamana na mke wake, David anaondoa sehemu ya mshahara wake kwenye akaunti yake ya benki huko Gisenyi, nchini. Operesheni ambayo inamgharimu zaidi, lakini ndio chaguo lake pekee la kupata mapato yake kwa sasa: “Siku zote ni ngumu kidogo na kiwango cha uondoaji, benki hazifanani, lakini lazima tuwe na pesa taslimu. Tunatoa kwa faranga za Rwanda na kwenda kwenye ofisi ya kubadilisha fedha na ama kuzibadilisha kuwa dola au kuzibadilisha kuwa faranga za Kongo. Ni ngumu, lakini ndo hali yenyewe, tunalazimika kuishi hivyo! “

Mjini Goma, taasisi za benki zinasubiri idhini kutoka kwa mamlaka ya fedha nchini humo ili kufungua tena milango yao.