
Uchumi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado unastawi licha ya vita vya mashariki na mashambulizi ya kundi la waasi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda. Mjini Kinshasa, Waziri wa Fedha ametangaza jana, Alhamisi, Aprili 10, viashirio vikuu vya kifedha, vinavyoonyesha uthabiti fulani wa uchumi wa Kongo katika kukabiliana na hali ngumu ya usalama.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kulingana na Doudou Fwamba, waziri wa fedha wa DRC, kuendelea kukaliwa kwa maeneo makubwa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini kunasababisha hasara ya 4.5% ya mapato ya bajeti ya serikali. Ikiwa hali hii itaendelea, inaweza kuhatarisha uwekezaji uliopangwa katika ngazi ya kitaifa.
Hata hivyo, kiashirio cha kwanza kinaonyesha uthabiti fulani: kiwango cha ubadilishaji kimerekodi kushuka kidogo tu kwa 0.1% kati ya mwezi wa Januari na mwezi Machi 2025, ikilinganishwa na 4.2% katika kipindi kama hicho mwaka wa 2024.
Licha ya hali ngumu ya usalama, kiwango cha mfumuko wa bei kwa sasa kiko sawa karibu 10%, ikilinganishwa na 23% mnamo mwezi Juni 2024, wakati serikali ya sasa ilipochukua madaraka. Uboreshaji ambao waziri anahusisha na usimamizi mkali, sera za umma zinazoaminika na nidhamu kali ya bajeti.
Shirika lisilo la kiserikali nchi DRC la CREFDL, ambalo limebobea katika masuala ya fedha za umma, halipingi uchambuzi huu. Hata hivyo, linabainisha utulivu wa uchumi mkuuunaelezewa zaidi na ongezeko la mapato kutoka sekta ya madini.
Kuhusu mfumuko wa bei, serikali iliondoa haki fulani ili kupunguza athari kwa bei. Hata hivyo, CREFDL inatetea kanuni bora za kibajeti, hasa kwa kupunguza malipo chini ya taratibu za dharura.
Wakati shirika hili lisilo la kiserikali linabaini kwamba faida za kiuchumi bado hazijaonekana kwa raia, Waziri wa Fedha anasisitiza juu ya umuhimu wa kuongeza uwekezaji ili kuendeleza miundombinu ya uzalishaji.