DRC: Tunachokifahamu kuhusu utekaji wa M23 wa maeneo ya Kivu Kusini na Kaskazini

Wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametangaza kwamba wamerejesha udhibiti kusini mwa eneo la Lubero, katika milima ya Sake na Nyiragongo, kwa kuwabeba na kuwarudisha nyuma waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda.