
Bunge la Seneti limeanza kuchunguza ombi la kumvua kinga ya useneta rais wa zamani Joseph Kabila siku ya Alhamisi, Mei 15. Akishutumiwa na mamlaka ya Kongo kuwa mshiriki wa kundi la waasi la AFC/M23, mkuu huyo wa zamani wa nchi, ambaye sasa yuko uhamishoni, anakabiliwa na mashtaka mazito: uhalifu wa kivita, uhalifu dhidi ya binadamu, na mauaji ya raia. Maswali matatu ya kuelewa utaratibu huu ambao haujawahi kutokea ambao unaonekana kuwa mrefu na ngumu
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakikutana katika makao makuu ya Bunge, maseneta hao walilazimika kuchunguza mambo mengine kwenye ajenda kabla hata ya kushughulikia suala hili nyeti. Uchunguzi wa ombi la kumvua kinga rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila, ulipaswa kuanza kwa kusomwa kwa hati ya mashtaka iliyotumwa na mkaguzi mkuu wa FARDC, ambapo mashtaka dhidi ya rais huyo wa zamani yanawekwa wazi.
Joseph Kabila anatuhumiwa nini?
Wanachama wawili wa serikali wamezungumza katika wiki za hivi karibuni kumkosoa moja kwa moja Rais wa zamani Joseph Kabila. Jacquemain Shabani, Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani, na Constant Mutamba, Waziri wa Sheria, wanamtuhumu kwa kushiriki kikamilifu katika vita mashariki mwa DRC, anakumbusha mwandishi wetu wa habari kutoka kitengo Afrika Patient Ligodi.
Félix Tshisekedi mwenyewe, Rais wa sasa wa Jamhuri, alikwenda mbali zaidi kwa kusema hadharani kwamba Joseph Kabila nichanzo cha AFC/M23, kundi lenye silaha ambalo linadhibiti miji na vijiji kadhaa katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini.
Je utaratibu utafanyikaje?
Kwa upande wa mahakama, wako tayari kwa hali yoyote. Waziri Constant Mutamba amesema kuwa kesi hiyo ni nzito na kutangaza kuwa mali zote zinazotambulika za rais huyo wa zamani, zikiwemo akaunti na mali zake za benki, zitakumbwa na hatua za kukamatwa. Lakini kabla ya hapo, utaratibu wa bunge lazima ufuate mkondo wake.
Maelezo kamili ya kikao hicho bado hayajajulikana, kutokana na hali ambayo haijawahi kushuhudiwa, anaeleza mwandishi wetu wa Kinshasa, Paulina Zidi. Inawezekana kwamba maswali yataulizwa na maseneta na chaguo la kikao cha faragha halijafutiliwa mbali. Kulingana na vyanzo vilivyo karibu na afisi ya Bunge la Seneti, kamati ya kiufundi inaweza kuundwa ili kuendeleza uchunguzi wa kina, kabla ya uwezekano wa mjadala katika kikao cha mashauriano na kufuatiwa na kura. Tume hiyo pia inatarajiwa kumsikiliza Joseph Kabila, lakini kwa sasa yuko nje ya nchi.
Uamuzi huo utafanywa lini?
Tarehe ya uamuzi wa mwisho itategemea afisi ya Bunge la Seneti. Ikiwa tume itaundwa kweli, itakuwa na siku chache kutoa matokeo yake. Haya basi yangewasilishwa kwa maseneta wote kwa kura katika kikao cha mashauriano, ambapo uamuzi wa mwisho utachukuliwa.
Lakini hata kama unge la Seneti lingeidhinisha kuondolewa kwa kinga, mchakato huo bado haujakamilika. Kwa sababu Joseph Kabila ni seneta wa maisha na rais wa zamani wa Jamhuri. Hata hivyo, kuondolewa kwa kinga kwa mkuu wa zamani wa nchi kunahitaji idhini kutoka kwa Baraza la Congress, ambayo ni, mkutano wa pamoja wa vyumba viwili vya Bunge. “Hatuwezi kutenganisha hadhi hizi mbili,” anaelezea mtaalamu aliyehojiwa na RFI, ambaye anasisitiza kuwa vyovyote itakavyokuwa leo, mchakato bado utakuwa mrefu.