DRC-Rwanda: Mchakato, ukiongozwa kwa sehemu na Washington, kupelekea kusainiwa kwa mikataba 3

Hatua mpya katika mchakato unaoendelea wa kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC imefanyika siku ya Ijumaa, Mei 2, 2025, mjini Washington, wiki moja baada ya kusainiwa kwa tamko la kanuni kati ya mawaziri wa mambo ya nje, mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Kinshasa na Kigali kila moja ilitakiwa kuwasilisha, ifikapo Mei 2, vipengele vitakavyojumuishwa katika rasimu ya awali ya makubaliano ya amani. Hakuna mawasiliano yaliyofanywa na wajumbe hao wawili, ambao bado walikuwa wakifanyia kazi nakala zao jioni ya Mei 2. Mchakato huu wa kidiplomasia, ukiongozwa kwa sehemu na Washington, bado haujakamilika. Ni hatua katika mchakato unaojumuisha angalau mikataba mitatu.

Mei 2 iliashiria awamu muhimu katika kujaribu kutatua mzozo mashariki mwa DRC, lakini mchakato bado unaendelea. Rasimu ya awali ya makubaliano ya amani ilipaswa kuwasilishwa. Kisha  itachunguzwe na wataalam wa Kongo, Rwanda na Marekani.Rasimu hii ilipaswa kuendana na tamko la kanuni lililotiwa saini wiki moja mapema. Itafuata pointi kuu zilizoainishwa: uhuru wa eneo, mapambano dhidi ya vmakundi yenye silaha, biashara ya madini, suala la wakimbizi, ushirikiano wa kikanda na jukumu la vikosi vya kimataifa, haswa MONUSCO.

Sauti kadhaa zimepazwa wiki hii zikitaka kuwepo kwa uwazi zaidi na ushirikishwaji katika mijadala hii chini ya uongozi wa Marekani. Kwa Profesa Martin Ziakwau Lembisa wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Kongo, ambaye maoni yake yalikusanywa na Alexandra Brangeon wa kitengo cha RFI kanda ya Afrika, tatizo la msingi tayari ni uwazi unaozingira mijadala inayohusisha mataifa.

“Tunaona kwamba hatua ya kuanzia sio kutambuliwa kwa uchokozi wa Rwanda dhidi ya DRC. Kwa hivyo, tunapuuza ukweli usiopingika na tunataka kujenga ukweli mwingine kwa kuzingatia mazingatio mengine, kimsingi ya hali ya kiuchumi. Ndio, tunaweza, kwa kuzingatia ukweli huu mpya, kwa shinikizo kutoka Marekani, kupata kuobdka kwa wanajeshi wa Rwanda kutoka eneo DRC, na mwisho wa harakati za M23, haka kama itakumbukwa kwamba M23 sio kundi pekee lenye silaha mashariki mwa DRC.

Kwa hiyo, hii ina maana kwamba hii haitoshi kutatua tatizo la msingi. Lakini hata hivyo, hii inaweza kuwa haitoshi ili kuhakikisha utulivu wa kudumu. Walakini, tunachohitaji ni kuunda mazingira ya azimio la kina la hali hiyo kwa suluhisho la kudumu. Lakini kama, katika harakati hizi za kutafuta hakikisho la usalama kwa Rwanda, kuna uwazi, kwa kuwa hakuna mawasiliano ya wazi juu ya jambo hili, hilo tayari linaleta tatizo.”

Mikataba mitatu yatarajiwa

Mikataba mitatu inatarajiwa katika hatua hii kama sehemu ya upatanishi unaoongozwa na Marekani. Mkataba wa kwanza ni wa amani kati ya DRC na Rwanda, unaotarajiwa kutiwa saini mwezi Juni. Wakati huo huo, mikataba miwili ya kiuchumi baina ya nchi mbili lazima ikamilishwe na Washington.

Wa kwanza inahusu DRC. Unatoa uwekezaji wa mabilioni ya dola na makampuni ya Marekani katika migodi ya Kongo na miundombinu inayohusiana.

Mkataba wa pili kwa Rwanda. Unahusu ukuzaji wa uwezo wa usindikaji, uchenjuaji na uuzaji wa madini. Si muhimu kwa kiasi kuliko ile iliyotiwa saini na DRC, lakini inasalia kuwa muhimu katika usanifu wa jumla wa ushirikiano, kulingana na chanzo cha kidiplomasia.

Kipengele cha ushirikiano kati ya Kinshasa na Kigali pia kinajadiliwa, kuhusu uchimbaji wa thamani wa madini. Madini yanayochimbwa nchini DRC yanapaswa kupitishwa kihalali kupitia Rwanda, ili kuchakatwa, kusafishwa na kusafirishwa hadi Marekani. “Tunaweza pia kufikiria kwamba DRC pia itahusika katika kusafisha na kuongeza thamani ndani ya makampuni yaliyoanzishwa nchini Rwanda. “Hakutakuwa na pande itakayopoteza,” kinaongeza chanzo cha kidiplomasia.

“Mchezo wa Marekani”

Mikataba hii mitatu, ya kisiasa na kiuchumi, inategemeana, na yaliyomo bado yako mbali kukamilika. Wiki hii, sauti kadhaa zilipazwa dhidi ya “mpango huu wa Marekani” ambao ungehusisha uwekezaji dhidi ya usalama mashariki mwa nchi. Wengine wanaona kuwa ni uuzaji wa maliasili za nchi. DRC inaweza, hata hivyo, kunufaika kiuchumi kutokana na mpango huu, anabaini Profesa Martin Ziakwau Lembisa wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Kongo.

Kuvutia uwekezaji wa Marekani kutachangia kiuchumi, hasa kwa kutoa ajira kwa Wakongo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *