
Vyombo vya usalama vya Kongo na Naibu Waziri Mkuu anayehusika na Mambo ya Ndani walifanya vikao kadhaa mwishoni mwa juma lililopita mjini Kinshasa. Vikao hivi vililenga kufafanua uwezekano wa uhusiano kati ya baadhi ya wadau wa kisiasa na kidini na makundi yanayoweza kutishia usalama wa taifa, katika muktadha unaoashiria kusonga mbele kwa waasi wa AFC/M23 mashariki mwa nchi, kinaeleza chanzo cha serikali.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Viongozi wawili wakuu walisikilizwa: Emmanuel Ramazani Shadary, katibu mkuu wa PPRD, chama cha rais wa zamani Joseph Kabila na Askofu Donatien N’shole, katibu mkuu wa Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini DRC, CENCO.
Nchini DRC, Emmanuel Ramazani Shadary alihojiwa kwa karibu saa moja na nusu. Mbelr yake walikuwa maafisa kadhaa wakuu wa usalama: mkuu wa idara ya ujasusi (ANR), mkurugenzi mkuu wa idara ya Uhamiaji (DGM) na Naibu Waziri Mkuu wa Mambo ya Ndani.
Taarifa kwa vyombo vya habari ya aliyekuwa spika wa Bunge la taifa, Aubin Minaku, ilikuwa katikati ya majadiliano. Aubin Minaku alitangaza hadharani: “Hakuna siri tena, hakuna shughuli za siri tena.” Ramazani Shadary alieleza kuwa huu haukuwa wito wa vitendo visivyo halali bali ni tangazo tu la shughuli za kisiasa.
Mada nyingine iliyojadiliwa ilikuwa uteuzi wa AFC/M23 kada wa zamani wa chama cha PPRD kama gavana wa mkoa wa Kivu Kusini. Wiki mbili mapema, Félix Tshisekedi alimshutumu mtangulizi wake Joseph Kabila kwa kuwa nyuma ya AFC/M23.
Kisha Askofu Donatien N’shole alisikilizwa. Ikiwa kwamba kuhojiwa kwake haikujatangazwa sana, Askofu Donatien N’shole alisikilizwa mbele ya mshauri maalum wa usalama wa mkuu wa nchi pamoja na mkuu wa idara ya ujasusi (ANR), mkuu wa idara ya uhamiaji (DGM) na polisi, kulingana na vyanzo mbalimbali.
Askofu Donatien N’shole alihojiwa kuhusu masuala mawili makuu
Idara ya usalama ilimhoji Monsinyo N’shole kuhusu masuala mawili makuu: mpango wa mazungumzo ulioongozwa na maaskofu wa Kikatoliki na wachungaji wa Kiprotestanti na shutuma za hivi majuzi za Baraza Kuu la Maaskofu wa kanisa Katoliki nchini DRC (CENCO) kuhusu vitendo vya unyanyasaji dhidi ya watu wanaozungumza Kiswahili mjini Kinshasa.
Kuhojiwa kwa viongozi hawa kunakuja siku chache baada ya kipindi kingine cha wasiwasi: Askofu N’shole kunyang’anywa pasipoti ya kusafiria na DGM huko Lubumbashi kwa zaidi ya saa moja. Tukio hili lilishutumiwa na CENCO.