Rais wa DRC Félix Tshisekedi, amemtaja moja kwa moja mtangulizi wake Joseph Kabila kwa kuwafadhili waasi wa M23 wanaoendelea kuvamia maeneo kadhaa ya mashariki mwa nchi hiyo, wakiungwa mkono na jeshi la Rwanda.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Tshisekedi alisema haya wakati akihudhuria kongamano la usalama mjini Munich nchini Ujerumani.
Sidhani kwamba upinzani ulioamua kuchukua silaha, na kuenda kuishirikisha Rwanda na kuja kuchochea mapinduzi haya dhidi ya Jamhuri, kwamba uko ndani ya haki yake. Ni wazi kuwa wafadhili wa kweli wanajificha, Na mfadhili halisi wa upinzani huu ni mtangulizi wangu, Joseph Kabila. amesema Félix Tshisekedi.
Tshisekedi ameongeza kuwa hata hivyo Kabila hakubali. Madai ambayo kambi ya Kabila inayakanusha mara moja.

Ferdinand Kambere, ni naibu Katibu mtendaji wa kitaifa wa Chama cha People’s Party for Reconstruction and Democracy (PPRD), anathibitisha kwamba kauli za Félix Tshisekedi zinaonyesha kukata tamaa kwake katika kukabiliana na mzozo wa usalama mashariki mwa DRC.
Kambere ameeleza kusikitishwa kuwa rais Tshisekedi wa sasa anamlaumu mtangulizi wake, wakati ambapo taifa linahitaji umoja kukabiliana na uchokozi wa Rwanda.