DRC: Rais atangaza hatua za kukabiliana na ongezeko la wizi na ghasia mjini Kinshasa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ongezeko la wizi wa kutumia silaha katika mji mkuu, Kinshasa, unatia wasiwasi mamlaka kuu nchini humo. Tukio jipya lilitokea Jumamosi, Juni 7, wakati Rais Félix Tshisekedi alizungumzia suala hilo wakati wa mkutano wa baraza la mawaziri, kulingana na kumbukumbu za mkutano wa serikali. Mkuu wa nchi wa Kongo alitoa wito wa kuhamasishwa kwa idara za usalama kukomesha hali hii, ambayo inatisha wadau wa masuala ya kiuchumi na wakaazi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Siku ya Jumamosi, Juni 7, saa moja jioni, lori lililokuwa limembeba raia wa China na dereva wake lilikuwa linatokea benki kando ya barabara kuu ya Lumumba Boulevard mjini Kinshasa. Karibu na kiwanda kimoja, watu watatu wenye silaha waliokuwa kwenye pikipiki walishambulia gari hilo na kumpiga risasi dereva, raia wa Kongo.

Tukio hilo lililonaswa na CCTV lilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama.

Siku chache mapema, umbali wa kilomita moja, majambazi wapatao kumi na watano walivamia kitengo cha kuhifadhia bidhaa za chakula katika mtaa wa Lemba mchana kweupe.

Ujambazi unazidi kuwa tukio la karibu kila wiki mjini Kinshasa. Wahalifu hao, mara nyingi wakiwa kwenye pikipiki, wanafanya uhalifu wao bila woga mbele ya watu wote, wakati mwingine wakirekodiwa na mashahidi. Kutokana na ongezeko hili, rais Félix Tshisekedia alitoa wito wa uhamasishaji wa jumla wa vikosi vya usalama kwa ajili ya “majibu ya nguvu, ylioratibiwa na endelevu.”

Miongoni mwa hatua zilizotangazwa: doria zaidi, kuongezeka kwa ufuatiliaji katika maeneo nyeti, na ongezeko linaloonekana la idadi ya maafisa wa polisi na wanajeshi katika vitongoji hatarishi na maeneo ya biashara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *