
Kutokana na ongezeko la ukosefu wa usalama, waasi wa AFC-M23 wamekuwa wakifanya operesheni za “kufunga” na kufanya msako katika wilaya mbalimbali za mji mkuu wa Kivu Kaskazini, na pia katika mji wa Saké tangu mwishoni mwa juma lililopita. Wakati vuguvugu hilo likidai kuwa limefanikiwa kuwakamata karibu watu 300 katika muda wa siku tatu na linataka kuwakamata watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria, baadhi ya mashirika ya kiraia yanalaani aina hiyo ya “msako”.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Operesheni za “kufunga” na kufanya msako katika wilaya mbalimbali za mji mkuu wa Kivu Kaskazini, na pia katika mji wa Saké tangu Jumamosi, Mei 10, zinalenga vitongoji vilivyoathiriwa zaidi na ukosefu wa usalama – haswa vile vya kaskazini na magharibi mwa mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini – ambapo mauaji kadhaa yamerekodiwa katika wiki za hivi karibuni, pamoja na kuongezeka kwa idadi visa vya wizi na utekaji nyara. Siku ya Jumatatu, Mei 12, watu wanne wa familia moja waliuawa na kuchomwa wakiwa hai katika nyumba moja katika kijiji cha Kabale Katambi (Kansana), katika eneo la Nyiragongo, viungani mwa Goma.
Kwa mujibu wa AFC-M23, operesheni zinazoendelea zinazolenga kuwakamata watu wote wanaomiliki silaha kinyume na sheria ili kukomesha ongezeko la uhalifu, zimesababisha kukamatwa kwa askari zaidi ya 200 wa Kongo, karibu wapiganaji mia moja Wazalendo, wanaoshukiwa kuwa wanachama wa FDLR na wahalifu 154, lakini kiwango chao na mbinu iliyotumika imezua utata na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashirika ya kiraia.
“Ni lazima kusitisha operesheni hii ya kusaka watu”
“Hawakamatiki watu kwa msingi wa vitu vya kijeshi au alama maalum: wanachukua vijana wote ambao bado wana umri wa kuinukia!” Wengine walichukuliwa siku tatu zilizopita na bado hawajarudi… Lakini kuwakamata watu kiholela bila sababu za kisheria ni ukiukwaji wa haki za binadamu, anasema Stewart Muhindo, mwanachama wa vuguvugu la Lucha, ambaye anasema hoja ya M23 ya usalama haihalalishi kila kitu. [Wapiganaji wa AFC/M23] hawana uwezo wa kuilinda Goma, lakini wakazi wa jiji hilo pia wanakabiliwa na ukosefu wa usalama kupitia utekaji nyara unaofanywa na wale wanaopaswa kulinda usalama wao, hiyo haukubaliki kabisa: kwetu sisi, kwa hiyo ni lazima kuwaachilia watu waliokamatwa na kukomesha operesheni hii ya kusaka watu,” ameongeza.
Wakati sauti nyingine ndani ya mashirika ya kiraia pia zinahofia kwamba kukamatwa huku kwa mfululizo kutasababisha kuajiriwa kwa lazima, Kinshasa na AFC/M23 zinalaumiana kuhusu kuongezeka kwa ukosefu wa usalama katika eneo hilo. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kongo, ambaye wiki iliyopita kwa mara nyingine tena alishutumu AFC/M23 kwa kukiuka utimilifu wa eneo la DRC na hivi karibuni kuwa na hatia ya zaidi ya kesi 300 za mauaji na mauaji ya kikatili, pamoja na takriban visa 100 vya ubakaji, mamlaka iliyowekwa na AFC/M23 katika mji wa Goma ilijibu hoja hiyo. Meya aliyeteuliwa na waasi alisema kuwa zaidi ya silaha 1,700 zimepatikana tangu kutekwa kwa Goma mwishoni mwa mwezi wa Januari, zikiwemo zaidi ya 300 katika siku za hivi karibuni.