DRC: Nini Kilichomo katika rasimu ya pili ya makubaliano ya amani kati ya Kinshasa na Kigali

Wajumbe kutoka DRC na Rwanda wanatarajiwa mjini Washington tena wiki hii. Lengo ni kuendeleza mazungumzo ya amani kati ya nchi hizo mbili.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nakala ambayo RFI imeweza kupata inakwenda mbali zaidi kuliko tamko la kanuni lililotiwa saini mwezi Aprili mwaka huu mjini Washington na mawaziri wa mambo ya nje wa Kongo na Rwanda. Katika waraka wa sasa, kutiwa saini kwa makubaliano ya amani kwanza kabisa ni Rwanda kujiondoa bila masharti katika ardhi ya Kongo. Hii ni pamoja na silaha na vifaa vilivyo chini ya udhibiti wa Rwanda, isipokuwa kesi zilizotolewa wazi kwa kwa tume ya mseto ya Kuratibu Usalama wa Pamoja.

Kwa mujibu wa habari zetu, hoja hii tayari ilitolewa katika mapendekezo ya Kongo ambayo yaliunda msingi wa rasimu ya kwanza. Tatizo: Kigali haijawahi kukiri kuwepo kwa vikosi vyake nchini DRC. Serikali ya Rwanda badala yake inarejelea “hatua za kujihami” zilizowekwa kwa usalama wake.

Hali ya pili: kuondoa hali ya kuzingirwa huko Kivu Kaskazini. Kwa Sheria hiyo ambayo inatuma tangu mwaka 2021, kama ilivyo kwa mkoa wa Ituri, lazima itoe nafasi kwa utawala wa kiraia kuruhusu mchakato huo kuendelea. Hati hiyo pia inataja makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Kinshasa na M23, ambayo bado yanajadiliwa chini ya mwamvuli wa Doha. Mantiki iko wazi: makubaliano na Rwanda yanaweza tu kusainiwa baada ya kukamilika kwa makubaliano kati ya Kinshasa na AFC/M23.

Mswada huo wa makubaliano pia unazungumzia suala la kundi la waasi wa wa Kihutu wa Rwanda la Democratic Forces for Liberation of Rwanda (FDLR). Nchi hizo mbili lazima “ziratibu kwa nia njema kutambua, kutathmini, kupata na kukomesha uwepo wa waasi wa FDLR.” Ushirikiano huu ni sehemu na kwa mujibu wa masharti ya Dhana ya Uendeshaji iliyokubaliwa huko Luanda mnamo Oktoba 2024. Maandishi hayo pia yanaeleza kuwa DRC itakataza na kuzuia usaidizi wowote wa vifaa au wa kifedha, uwe wa kitaifa au wa kigeni, unaokusudiwa kwa FDLR.

Iwapo hati itatiwa saini, ahadi zitatumika katika eneo lote, ingawa Kivu Kaskazini na Kusini zitasalia kuwa kiini cha mpango huo. Lakini hii ni rasimu tu. Kazi halisi ya mazungumzo inaanza wiki hii. Inaweza kusababisha mkutano wa mawaziri kabla ya uwezekano wa kutiwa saini na marais wa DRC na Rwanda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *