
Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu inaishutumu moja kwa moja M23 kwa kuwakamata watu wasiopungua 130 katika hospitali mbili huko Goma, moja ya miji mikuu mashariki mwa DRC, ambayo sasa inadhibitiwa na kundi la waasi la M23, linaloungwa mkono na Rwanda. Umoja wa Mataifa unakumbusha kuwa hospitali lazima ziheshimiwe na kulindwa, chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Coralie Pierret
Ilikuwa saa 9usiku wakati wapiganaji kadhaa waliingia katika hospitali ya CBCA ya Ndosho, huko Goma, usiku wa Machi 2 kuamkia 3. Wauguzi au ndugu wa wagonjwa waliokuwa wanaotibiwa na baadhi ya watu waliojeruhiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa, walichukuliwa na kuingizwa katika gari ndogo ya jikeshi aina ya jeep. Watu 116 kwa jumla kulingana na Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu, takwimu iliyothibitishwa na chanzo cha ndani, wanaume pekee, wanapelekwa kusikojulikana, vyanzo kadhaa vimesema.
Kati ya Februari 28 na Machi 1usiku, tukio kama hilo lilitokea katika hospitali nyingine ya Heal Africa huko Goma. Watu kumi na watano walikamatwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.
Kundi la waasi la M23 linahusishwa
Katika visa vyote viwili, Umoja wa Mataifa unanyooshea kidole M23. Katika vituo hivi viwili vya afya, majeruhi kadhaa wa vita wanatibiwa, wakiwemo wanajeshi kutoka jeshi la Kongo na Wazalendo, wanamgambo wanaoiunga mkono serikali. Hao ndio waliolengwa, Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu inabaini.
Kundi la M23, ambalo limedhibiti jiji hilo tangu mwisho wa mwezi wa Januari, halijathibitisha kukamatwa kwa mtu yeyote. Hata hivyo ikumbukwe kwamba Wazalendo na wanajeshi wanatafutwa “kurejeshwa katika maisha ya kiraia au kurejeshwa jeshini”, yaani waweke silaha chini au wajiunge na kundi lao. Kabla ya kuwasili mjini humo, kundi hilo lenye silaha lilikuwa limetoa amri kwa wanajeshi na wanamgambo wa Kongo kuweka chini silaha zao.