DRC na Marekani zajadili makubaliano ya baadaye ya uchimbaji madini

Mkataba wa uchimbaji madini kati ya DRC na Marekani kwa sasa unajadiliwa. Huu bado si mkataba uliotiwa saini, lakini mfumo unaojadiliwa, unaonuiwa kuvutia uwekezaji zaidi wa Marekani katika sekta ya madini ya Kongo. Kulingana na utawala wa Trump, mradi huu ni sehemu ya mkakati wake wa kiuchumi kwa bara la Afrika. Lakini ni jinsi gani mpango huu unachukuliwa kuwa thabiti kutoka kwa mtazamo wa Marekani?

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkataba huu kati ya DRC na Marekani ni kuwezesha makampuni ya Marekani kuwekeza katika uchimbaji madini wa Kongo, lakini pia katika miundombinu muhimu, kama vile barabara, reli, mabwawa na nishati.

Serikali ya Marekani haisimamii migodi moja kwa moja, lakini inarahisisha uwekezaji kupitia taasisi kama vile DFC au Benki ya EXIM. Marekani inasisitiza kuwepo kwa ushirikiano wa “manufaa kwa wote, kuheshimu sheria za ndani na kimataifa, hasa katika masuala ya mazingira, kazi na mapambano dhidi ya rushwa.

China imeimarika vyema nchini DRC

Lakini mradi huu unakuja katika muktadha fulani. China leo ndiyo mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa DRC. Inawakilisha zaidi ya nusu ya mauzo ya nje ya Kongo, na karibu nusu ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje. Kwa kiasi kikubwa inatawala sekta ya madini.

Katika mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini, makampuni ya China pia yanashutumiwa mara kwa mara kwa kutumia dhahabu na madini mengine kinyume cha sheria, mara nyingi kuhusiana na mitandao ya magendo. Inabakia kuonekana jinsi Marekani inanuia kuingia katika mazingira haya tata, hasa katika maeneo yasiyo imara. Katika hatua hii, Washington bado imesalia kimya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *