
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mvutano unaendelea kati ya Bunge la taifa na Mahakama ya Katiba kuhusu kesi ya waziri mkuu wa zamani Matata Ponyo Mapon. Waziri mkuu huyu wa zamani ambaye sasa yuko katika upinzani anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma: karibu dola milioni 200 zilizokusudiwa kuanzishwa kwa Hifadhi ya chakula ya Bukangalonzo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa
Katika kesi yake mwezi uliopita, upande wa mashtaka uliomba kifungo cha miaka 20 jela. Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Waziri Mkuu huyo wa zamani aliomba kinga yake ya ubunge. Na mjadala huo umezidi kushika kasi katika siku za hivi karibuni kati ya spika wa Bunge na mkuu wa Mahakama ya Katiba.
Matata Ponyo alipofikishwa mbele ya Mahakama Kuu, alikuwa seneta na kinga yake ilikuwa tayari imeondolewa. Tangu wakati huo, kesi hiyo imechukua mkondo wake na kbadilika mara kadhaa. Mwishoni mwa mwaka 2023, mkuu wa zamani wa serikali alichaguliwa kuwa mbunge wa kitaifa na hivyo kupata kinga mpya ya bunge. Kesi iliporejelewa mwezi Aprili mwaka jana, Aliombwa kufika mahakamani na alikataa kufika. Lakini Mahakama imeamua kuendelea na kesi hiyo.
Hakuna kurudi nyuma
Kwa hiyo Spika wa Bunge alimejiweka kwenye mjadala huo. Vital Kamerhe ameiomba Mahakama kuheshimu utaratibu na kuomba kuondolewa upya kwa kinga hiyo. Majibu kutoka kwa Mahakama ya Katiba: hakuna suala la kurudi nyuma, Matata Ponyo tayari amefikishwa mahakamani, kesi zilifungwa mwishoni mwa mwezi Aprili. Na hukumu itatolewa Mei 14. Katika barua, Rais wa Mahakama amesisitiza kwa uthabiti uhuru wa mahakama.
Zikiwa zimesalia siku tisa, Mahakama ya Katiba ya DRC kwa hiyo inapaswa kutoa uamuzi. Kiongozi wa upinzani na mkuu wa zamani wa serikali anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka ishirini kwa tuhuma za ubadhirifu wa karibu dola milioni 200.