DRC: Mwendesha mashtaka wa ICC awasili Kinshasa kwa ajili ya uchunguzi wa ghasia Kivu Kaskazini

Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) yuko katika mji wa DRC, Kinshasa, tangu Jumatatu jioni, Februari 24. Karim Khan anatarajiwa kukutana na viongozi wa Kinshasa ili kujua kinachohitajika kufanywa na ICC, kuhusiana na matukio ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Ziara hiyo inakusudiwa kuwa onyo kwa wahusika wa uhalifu unaotekelezwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Hague, Stéphanie Maupas

Mwendesha mashtaka anatarajiwa kukutana na vongozi wa Kongo, kuanzia na mkuu wa nchi, Félix Tshisekedi, na wajumbe wa serikali. Karim Khan pia ana miadi na Bintou Keita, mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

Mwendesha mashtaka anakusudia kuifanya haki kuwa sehemu ya suluhisho la mzozo uliopo mashariki mwa DRC. Anatarajiwa kuwaonya wahusika wa uhalifu unaoendelea katika mko wa Kivu Kaskazini, ambapo M23, wanamgambo wanaoungwa mkono na Rwanda, wanapambana na jeshi la Kongo na wameteka sehemu kubwa ya mkoa huo.

Ni vizazi vingapi vya watoto wenu vitatolewa dhabihu? Je, watalengwa? Inatosha. Inatosha. Haya si machozi ya wanasheria, ni ya watoto, wanawake na wanaume wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hili si tatizo la kudharauliwa. Watu wengi sana wamekuwa wakiingilia mambo ya nchi hii kwa miaka mingi. DRC ina matatizo, ni kweli, lakini watu wamechagua amani, sio vita. Lakini kwa unyenyekevu wote unaohitajika, tunaunga mkono serikali ya DRC. Tunataka kuleta washirika wapya ili kujaribu kuanzisha mbinu thabiti, pana, endelevu na ya kiujumla ambayo itaondoa sumu ya uhalifu katika ardhi ya Kongo na ambayo itawawezesha watoto wenu kuwa na maisha bora ya baadaye baada ya siku hizi za hali ya sintofahamu ambazo mnaishi leo . Haitakuwa rahisi. Tukishirikiana kwa dhana kwamba watoto hawa ni watoto wetu, kwamba familia zinazoteseka ni zetu, hatutaruhusu hili liendelee.

“Watu wengi wameingilia mambo ya nchi hii kwa miaka mingi”, ameongeza Karim Khan.

Mapema mwezi huu, Mwendesha Mashtaka alitoa wito kwa mashahidi. Kama ilivyo katika uchunguzi wote, atahitaji ushirikiano wa Mataifa, kwanza kabisa ushirikiano kutoka DRC.

Karim Khan alifungua uchunguzi huu katika mkoa wa Kivu Kaskazini mwezi Oktoba mwaka uliyopita kwa ombi la mamlaka ya Kongo. Uchunuzi huo unashughulikia uhalifu uliofanywa katika mkoa huo tangu Januari 1, 2022.

Mbali na uchunguzi huu, ofisi yake pia inakusudia kuunga mkono kuundwa kwa mahakama maalum nchini DRC.