Mkuu wa jeshi nchini Uganda, Muhoozi Kainerugaba, amedai jeshi la Uganda, UPDF au waasi wa M23 watawasili katika mji wa Kisangani nchini DRC chini ya juma moja lijalo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kainerugaba ambaye pia mwana wa rais Yoweri Museveni, amesema jeshi lake au waasi wa M23 watawasili Kisangani kwa agizo la rais Yoweri Museveni ili kuwaokoa wakaazi wa Kisangani, chini ya juma moja lijalo.
Wanajeshi wa Uganda wapo nchini DRC, kwa ushirikiano na jeshi la FARDC, kupambana na makundi mengine ya waasi likiwemo lile la CODECO.

Si mara ya Kwanza kwa mkuu huyo wa jeshini Nchini Uganda kutoa kauli za kutatanisha kwa kutumia mtandao wake wa X, juma lililopita Keinerugaba alikutana na rais wa Rwanda Paul Kagame, ambaye amekuwa akituhumiwa kuwaunga mkono waasi M23, kutatiza usalama mashariki mwa DRC.
Licha ya waasi wa M23 kuwasili katika miji kadhaa ya mashariki mwa DRC, waasi hao hawajaonesha nia ya kutaka kudhibi jiji la kimkakati la Kisangani, M23 ikidai inapanga kujiondoa katika mji wa Walikale ili kutoa nafasi ya mazungumzo na serikali.