Shirika la Kimataifa la Madaktari Wasio na Mipaka, MSF, juma hili limesema raia wanauguza majeraha “ya kutisha” kutokana na ongezeko jipya la ghasia kwenye jimbo la Ituri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mji wa Ituri ambao ina utajiri mkubwa wa madini, kwa muda mrefu umeshuhudia makabiliano kati ya wanamgambo wa kikabila pamoja na mashambulizi ya kundi lenye uhusiano na Islamic State, Allied Democratic Forces (ADF).
MSF imesema kwenye taarifa yake kuwa, limerekodi ongezeko kubwa la vitendo vya ukatili katika jimbo la Ituri, ambapo wataalamu Wake wa afya wamekuwa wakitoa huduma kwa raia wenye majeraha ya kutisha”.

Ikinukuu takwimu za Umoja wa Mataifa, shirika hilo limesema ghasia zimewakosesha makazi takriban watu laki 1 tangu mwanzoni mwa mwaka, huku mashambulizi yakiua zaidi ya watu 200 mwezi Januari na Februari pekee.
MSF inasema vituo vya afya vimekuwa vikilengwa na kwamba vitisho toka kwa makundi yenye silaha vimesabahisha baadhi ya hospitali kusitisha huduma na kuwahamisha wagonjwa.