DRC: Misaada ya kibinadamu iko hatarini kutokana na ukosefu wa ufadhili wa kimataifa

Mpango wa kukabiliana na mzozo wa kibinadamu nchini DRC ulifanyika Alhamisi, Februari 27, 2025 mjini Kinshasa ili kujaribu kukusanya fedha kutoka kwa wafadhili wa kimataifa. Hata hivyo, licha ya mzozo unaozidi kuwa mbaya mashariki mwa nchi hiyo, fedha zinazokusanywa huenda zikawa ndogo kuliko mwaka jana kutokana na kupungua kwa ufadhili wa Marekani kwa ajili ya misaada ya kimataifa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Coralie Pierret

Huko Kinshasa, mji mkuu wa DRC, uwasilishaji wa mpango kwa majibu ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2025 ulifanyika siku ya Alhamisi, Februari 27, kwa lengo la kukusanya dola bilioni 2.54 kutoka kwa wafadhili wa kimataifa. Hata hivyo, bahasha hii itakuwa ngumu zaidi kuipata kuliko miaka ya nyuma kutokana na mzozo wa kimataifa wa kifedha unaohusishwa na kuzuiwa kwa msaada wa Marekani.

Kazi ngumu zaidi ya kibinadamu

Kwenye jukwaa, hotuba zilifuata moja baada ya nyingine, na kila mtu alikubaliana juu ya uzito wa mgogoro huo. Ukweli mpya, kama vile kutekwa kwa iji ya Goma na Bukavu na AFC/M23, kundi lenye silaha linaloungwa mkono na Rwanda, kunatatiza kazi ya mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo dhaifu sana.

Benki na viwanja vya ndege vya Goma na Bukavu vimefungwa, na kuzuia usambazaji wowote, maghala ya misaada ya kibinadamu yaliporwa wakati wa kutekwa kwa miji hii miwili muhimu zaidi Mashariki mwa DRC, watu kuyatoroka makazi yao, haswa kuelekea Burundi, idadi ambayo bado ni ngumu kutathmini leo… Hizi ndizo changamoto kuu ambazo mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakikabiliana nayo tangu mwisho wa mwezi wa Januari.

Luc Lamprière, mkurugenzi wa Jukwaa la mashirika ya Kimataifa yasiyo ya kiserikali nchini DRC, anakumbusha: “Tunakabiliwa na migogoro mingi kwa wakati mmoja. Wafadhili wa kibinadamu wanakabiliwa na shida za mara kwa mara na zisizowezekana: jinsi ya kutibu waliojeruhiwa wakati hospitali hazina kila kitu? Tunawezaje kuzuia maafa ya kiafya wakati kipindupindu, surua na Mpox vinaendelea kuenea? Jinsi ya kuwalinda waathirika wa unyanyasaji wa kijinsia, watu waliohamishwa wanaoishi kwa hofu? “

Ufadhili mdogo

Je, tunawezaje pia kukidhi mahitaji haya wakati ufadhili haupo? Matangazo ya kupunguzwa kwa bajeti yamekuwa yakimiminika tangu kusitishwa kwa msaada wa Marekani. Joakim Vaverka, balozi wa Sweden nchini DRC na mwakilishi wa wafadhili, anaeleza: “Tunajikuta katika hali mbaya sana. Wakati huo huo, ni mzozo uliosahaulika: kwa kuzingatia zaidi mzozo huu, inaweza kuwa fursa kwa wafadhili kuongeza ushiriki wao. “

Kwa wasaidizi wa kibinadamu, suluhu bora la mzozo huo si msaada, bali ni utatuzi wa mzozo huo na mchakato wa amani endelevu.

“Utatuzi wa kisiasa wa mzozo ungekuwa na athari za haraka”, amesema Bruno Lemarquis, mratibu wa masuala ya kibinadamu wa operesheni za Umoja wa Mataifa nchini DRC.