
Milipuko miwili imesikika siku ya Alhamisi, Februari 27, kwenye eneo la Uhuru huko Bukavu, wakati Corneille Nangaa, mratibu wa AFC/M23, alipokuwa akimaliza mkutano wake. Kulingana na vyanzo vya RFI, takriban watu saba waliuawa. Hii ni idadi ya muda. Asili ya milipuko bado haijulikani katika hatua hii. Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini, iko chini ya udhibiti wa AFC/M23, vuguvugu la kisiasa na kijeshi linaloungwa mkono na Rwanda, tangu Februari 14.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Dakika mbili baada ya Corneille Nangaa kumaliza mkutano wake, mlipuko wa kwanza ulisikika. Inaonekana umetoka eneo ambalo vipaza sauti vilikuwa wimwekwa, karibu mita nne kutoka kwenye ukumbi.
Wakati huo huo umati wa watu walitawanyika pande zote: kelele, machozi, msongamano. Kisha, mlipuko wa pili ukasikika. Miili kadhaa imeonekana baada ya milipuko hiyo. Papa hapo miili ya watu watano imeonekana na wotewalikuwa wamevalia nguo za kiraia, kulingana na vyanzo vya RFI.
Wengi walijeruhiwa, wengine walikuwa chini, wengine wamehudumiwa haraka. Pikipiki za kiraia zimehitajika kusaidia kubeba majeruhi hospitalini, pia magari yamehamasishwa kusafirisha majeruhi hadi hospitali.
Shambulio bado halijafahamika
Lakini nini kilitokea? Asili ya milipuko bado haijajulikana kwa wakati huu. Mashahidi wanataja maguruneti, lakini hakuna kilichothibitishwa.
Kundi la waasi la M23 linaahidi kuzungumza wakati wa mchana. Lakini tayari linaishutumu Kinshasa kwa kuhusika na milipuko hii. Nani anawajibika? Swali linabaki wazi. Mji wa Bukavu nchini DRC uko katika hali ya wasiwasi.