DRC: Mchakato wa Doha umefikia wapi chini Qatar?

Wiki mbili baada ya Walikale-centre kudhibitiwa na vuguvugu la kisiasa na kijeshi la AFC/M23, waashi hao wamejiondoa katika mji huu katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini DRC. Kundi hilo lenye silaha linataja ishara ya kuunga mkono juhudi zinazoendelea za amani.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi 

Michakato wa kikanda inaonekana kukwama, lakini huko Doha, Qatar, upatanishi unaendelea. Nchi hiyo imefanikiwa kuwashawishi wajumbe kutoka kwa serikali ya Kongo na wale kutoka AFC/M23 kushirika kiao cha pamoja na inatumai kufikia usitishaji mapigano. Mchakato huu umefikia wapi kwa sasa?

Wajumbe hao walirejea katika makao yao makuu. Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia, walipaswa kurejea Doha wiki moja baadaye. Hata hivyo, hadi sasa, hakuna mwaliko rasmi ambao umetolewa na maelezo ya vifaa hayajawasilishwa.

Masharti 

Kulingana na vyanzo hivyo, AFC/M23 imewasilisha masharti yake. Awamu ya kwanza iliyofanyika Doha haikutoa matokeo yoyote madhubuti. Kulingana na vyanzo vilivyo karibu na faili hiyo, swali lingine lilihusu jukumu lililopewa ujumbe wa Kinshasa, na haswa uwezo wake wa kufanya maamuzi, ambao kimsingi unajumuisha maafisa wa kijasusi na wanajeshi.

Kwa mujibu wa RFI, maafisa wa Rwanda pia wamealikwa kwa mara nyingine tena Doha. Kulingana na afisa wa Rwanda, haya hayakuwa majadiliano kati ya AFC/M23, serikali ya Kongo na Rwanda, lakini ni ufuatiliaji wa mkutano wa Machi 18 mjini Doha kati ya wakuu wa nchi za Kongo, Rwanda na Qatar.

Mazungumzo ya siri

Mbinu mbili tofauti, chanzo hiki kinabainisha. Hata hivyo, imethibitishwa kuwa Doha inahitaji usiri mkubwa. Sharti ambalo ni kubwa zaidi kwa kuwa, barani Afrika, upatanishi huu unapokelewa kwa shingo upande. Kenya, Angola na mataifa mengine ya Afrika yanayoshiriki katika juhudi za amani katika kanda ya Maziwa Makuu zimetoa maoni machache kuhusu mpango huo wa Qatar. Wanadiplomasia kadhaa wanaonyesha kuwa nchi hizi zinasalia kushikamana na kanuni ya “suluhisho za Kiafrika kwa matatizo ya Kiafrika.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *