
Serikali ya Kinshasa, hivi leo inatarajiwa kuzindua rasmi mazungumzo ya kitaifa kwa lengo la kuunda Serikali ya umoja, majadiliano haya yakifuatia tangazo la rais Felix Tshisekedi alilolitoa mwezi uliopita.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Katika hotuba yake rais Tshisekedi, alisema serikali itakayoundwa itakuwa na jukumu la kuwaunganisha raia na kukabiliana na changamoto za usalama mashariki mwa nchi hiyo.
Majadiliano haya yataweka pamoja wa Kongomani wanaojihusisha kuheshimu kanuni zilizofafanuliwa hapa na Espoir Masamanki, Kiongozi wa ofisi ya mshauri maalum wa rais kuhusu usalama, ilikushiriki majadiliano hayo.
“Mashauriano hayo yamejikita katika misingi kadhaa muhimu ikiwa ni pamoja na ukuu wa kikatiba na heshima kwa taasisi zilizoanzishwa kikatiba.” alisema Espoir Masamanki.
Kwa mujibu wa Profesa Masamanki, makundi manne ya washiriki ndiyo wanalengwa kwa majadiliano haya hata pia Rais mustaafu Joseph Kabila.
“Watakaoshiriki ni wa wabunge kutoka Muungano wa Sacred Union, vyama vya upinzani walio ndani ya wabunge na nje mabunge, asasi za kiraia wote kwa jumla, kama vile madhehebu ya dini, watu huru wakiwemo waliokuwa wagombea kwa urais, viongozi wa umma na watu mashuhuri kutoka sekta mbalimbali.” Alieleza Profesa Masamanki.
Hata hivyo, chama cha Rais mustaafu Joseph Kabila PPRD, kimesema kimepokea pendekezo la Félix Tshisekedi, lakini hakitashiriki katika serikali mpya. Ferdinand Kambere, ni katibu naibu chama cha PPRD.
“La ni mitego yao kutaka kuwateka nyara watu.” alisema Ferdinand Kambere, ni katibu naibu chama cha PPRD.
Majadiliano haya yanalenga umoja wa kitaifa kama anavyotaka Raïs Tshisekedi, ambae alitoa wito waku maliza migogoro za ndani ili kukabiliana na vitisho toka nje, hasa mashariki mwa nchi.
Freddy Tendilonge/Kinshasa RFI Kiswahili