DRC: Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na M23 yaripotiwa kuendelea Doha

Mazungumzo kati ya serikali ya DRC na waasi wa AFC/M23 yanaripotiwa kuendelea jijini Doha nchini Qatar.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Licha ya vyanzo kutoka katika muungano wa waasi wa AFC/M23 na upande Joseph Kabila kuripoti kwamba rais huyo wa zamani wa DRC alitembelea Goma Ijumaa ya wiki hii, Marekani inasema inaendelea na juhudi zake kupunguza mzozo wa sasa.

Marekani inaripotiwa kuendelea kuweka shinikizo la kidiplomasia na kiuchumi kwa wahusika wote kwenye mzozo huo ikiwemo Kinshasa na Kigali.

Kulingana na vyanzo kwenye mazungumzo hayo jijini Doha, kwa kipindi cha siku nne, kinshasa na M23 hazijakutana moja kwa moja japokuwa zinawasiliana kupitia kwa wapatanishi wake.

M23 wajiondoa mjini Walikale, Kongo wakati huu wakitarajiwa kukutana nmjini Doha nchini Qatar
M23 wajiondoa mjini Walikale, Kongo wakati huu wakitarajiwa kukutana nmjini Doha nchini Qatar © @content stadium

Inaelezwa kwamba AFC/M23 inasisitiza kwamba inataka kutohusishwa katika mzozo wa DRC na nchi ya Rwanda.

Kwa upande wake Kinshasa inasema waasi wa AFC/M23 na utawala wa Rwanda wanaendelea kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji na utekaji wa vijana katika ardhi ya Congo hususan meneo ya Goma na Bukavu.

Mjadala huu ulichukua siku kadhaa, lakini kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari, maendeleo yamepatikana, kwani pande zote mbili zimeridhishwa. Taarifa ya pamoja imeandaliwa na hii ni kwa mujibu wa vyanzo vya RFI.

Joseph Kabila - Rais wa zamani wa DRC
Joseph Kabila – Rais wa zamani wa DRC REUTERS/ – Siphiwe Sibeko

Wahusika pia wanajadili yaliyomo katika maandishi. Kwa mfano, kwa mujibu wa taarifa zetu, Kinshasa inapendekeza kujumuishwa kwa makundi mengine yenye silaha kujiunga na mfumo wa kusitisha mapigano.

Hatimaye, mojawapo ya hoja nyeti zaidi inasalia kuwa “hatua za kujenga imani” zinazopaswa kutekelezwa, na ambao bado unafanyiwa kazi, amebainisha mwanadiplomasia mmoja kutoka nchi za magharibi huku kukiwa na matumaini ya kufikia mwafaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *