DRC: mashauriano kuhusu uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa yarejelewa

Serikali ya Jamhuriya Kidemokrasia ya Congo, inarejelea mashauriano ya kitaifa ya uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa, yaliyoanza wiki moja iliyopita, na kususiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa wa upinzani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais Felix Tshisekedi anaamini kuwa uundwaji wa serikali ya mpito, utasaidia kupatikana kwa suluhu kuhusu mzozo wa Mashariki mwa DRC, baada ya waasi wa M23 kudhibiti maeneo mbalimbali likiwemo jiji la Goma na Bukavu.

Mashauriano haya yanayoongozwa na kamati maalum inayomshauri rais Tshisekedi kuhusu masuala ya usalama, yanatarajiwa kumalizika wiki hii.

Tayari mashauriano hayo yamewahusisha watendaji wakuu serikalini na wiki hii, wabunge kutoka muungano wa siasa wa rais Tshisekedi, mashirika ya kiraia na baadhi ya viongozi wa upinzani wanatarajiwa kufikiwa.

Hata hivyo, vigogo wa upinzani, wakiongozwa na Martin Fayulu wamekataa mashauriano hayo, na uundwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa na badala yake wanataka viongozi wa dini kuachiwa jukumu la kuwaunganisha wananchi wa DRC katika kipindi hiki.

Naye Spika wa bunge la kitaifa, Vital Kamerhe, amesema mashauriano hayo, yasalie kwenye malengo yake ya kuunganisha upinzani na serikali, kwa lengo la kupata mwafaka wa ndani kuhusu mzozo wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *