
Rais wa DRC, Felix Tshisekedi, siku ya Alhamis alikutana na kiongozi wa upinzani Martin Fayulu, katika ikulu ya Palais de la Nation, mkutano uliokja siku chache kupita tangu Fayulu apendekeze wakutane kuzungumzia yanayoendelea nchini humo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu ambao ulikuwa unasubiriwa zaidi ulikuja siku tatu baada ya hotuba ya Martin Fayulu, ambapo alielezea nia yake ya kukutana na Rais Tshisekedi, ili kujadili mzozo wa usalama mashariki mwa nchi.
Kiongozi wa ECiDé alitoa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa kuhusu suala la uvamizi na kukaliwa na waasi wa AFC/M23 kwa miji miwili mikubwa, ambazo ni Goma na Bukavu.
‘‘Nchi iko katika kipindi kigumu sana. Tunashambuliwa kutoka kila mahali. Tunahitaji uwiano wa kitaifa. Nilikuja kumwambia kwamba hatuna suluhu 36. Ni lazima tuunde kambi kwa ajili ya nchi.Pamoja na machafuko haya yote tuliyo nayo, suluhu ni mazungumzo. Hatukupambana ili kesho Kongo igawanywe.’’ amesema Martin Fayulu.
Fayulu alimtaka pia Rais Tshisekedi kukutana na viongozi wa kidini, kutoka muungona wa ma askofu CENCO na wale wa Kanisa la Kristo nchini Kongo ECC, ambao wanapendekeza mapatano ya kijamii. Kulingana na Fayulu, Rais Tshisekedi aliahidi kujibu ombi hili kwa haraka.
Haya yanajiri wakati hali mashariki mwa nchi yaendelea kuwa mbaya kutokana na kuongezeka kwa mapigano kati ya wanajeshi wa Kongo na waasi wa M23.
Freddy Tendilonge/ Kinshasa/ RFI Kiswahili.