
Mapigano zaidi yameripotiwa kwenye vijiji vya Tchofui, Kasheke, Kabamba na Mabingu jimboni Kivu Kusini mashariki mwa nchi ya DRC kati ya wapiganaji Wazalendo na waasi wa AFC-M23 wanaosaidiwa na Rwanda.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Vyanzo vya kiusalama na mashirika ya kiraia kwenye mkowa huo, vimethibitisha kuwa wakaazi wa vijiji vya Tchofi na Kasheke wilaya ya Kalehe na vilevile Kabamba na Mabingu eneo la Kabare, wamejikuta katika hatari na wengine kulazimika kukimbia makazi yao.
Mapigano hayo yalianza Jumanne kwenye maeneo ya Kasheke-Lemera, katika eneo la Kalehe, ambapo vikosi pinzani vilipambana siku nzima.
Idadi kamili ya vifo kutokana na mapigano haya bado haijulikani, huku idadi ya watu waliolazimika kukimbia makazi yao inaongezeka na wengi wao hwana msaada wowote wa kibinadamu. Vyanzo vya ndani Vimesema.