
Mapigano mapya kati ya muungano wa wapiganaji wa Wazalendo-Mai-Mai na waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda, yameshuhudiwa katika kijiji cha Kampala-Bulambo, wilayani Wanyanga karibu na mji wa Walikale
Imechapishwa: Imehaririwa:
Matangazo ya kibiashara
Ripoti zinasema, wapiganaji wa Mai Mai wanaoshirikiana na Wazalendo walishambulia ngome ya M23 saa 11 Alfajiri siku ya jumatano, na kusababisha makabiliano makali.
Wakaazi wa eneo hilo na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameripoti maafa ila haijafahamika ni watu wangapi wamepoteza maisha.
Mapigano yameendelea kushuhudiwa, licha ya wito wa usitishwaji vita na jitihada za kikanda na kimataifa kujaribu kutafuta mzozo wa Mashariki mwa DRC.
Tangu waasi wa M23 wanaosaidiwa na Rwanda kuchukua miji muhimu ya Goma na Bukavu, pamoja na meeno mengine , Jumuiya za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika SADC wameendelea kushinikiza usitishwaji wa vita na mzozo huo kusuluhishwa kwa njia ya mazungumzo.