DRC: M23 na serikali ya Kinshasa zakubaliana kusitisha mapigano

DR Congo na waasi wa M23 wakubaliana usitishwaji wa vita mara moja, wakiahidi kuendelea na mazungumzo

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa ya pamoja, serikali ya DRC na waasi wa M23 wamekubaliana kusitisha uhasama hadi pale ambapo mazungumzo yatakamilika.

Serikali ya DRC na kundi hilo la waasi zimesema kipindi cha usitishwaji wa mapigano kitaendelea wakati huu zikiendelea kuufanyia kazi mchakato wa kuelekea kupatikana kwa mwafaka wa kudumu.

Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo yalioongozwa na nchi ya Qatar.

Makubaliano kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakionekana kutozaa matunda tangu mwaka wa 2021.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa na nchi za Magharibi zimekuwa zikieleza kwamba waasi wa M23 wanaungwa mkono na serikali ya Rwanda, ripoti ambayo Rwanda imeendelea kukanusha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *