DRC: Kwa kutamatisha mkataba wa uchimbaji madini, wabunge wa Marekani wnadai hakikisho la uwazi

Nchini DRC, mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kimkakati na Marekani katika sekta ya madini yanaibua mjadala unaokua. Kinshasa inatarajia kuhitimisha makubaliano haya haraka kwa matumaini kwamba yatawezesha ushiriki zaidi wa Washington katika kutafuta amani katika eneo la mashariki mwa nchi. 

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku tatu zilizopita, RFI ilifichua kuwa Rais Félix Tshisekedi alianzisha kitengo cha kimkakati kilichopewa jukumu la kufuatilia mijadala na kujiandaa kwa ajili ya utekelezaji wa makubaliano hayo. Lakini huko Washington, wajumbe watano wa Baraza la Congress wanadai ufafanuzi.

Hata huko Marekani, mashaka yanaanza kuonekana. Wajumbe watano wa Baraza la Congress wameandika barua kwa Massad Boulos, Mshauri Maalum wa White House kwa Afrika. Katika barua yao, wanauliza swali rahisi: Je, ni mambo gani yaliomo hasa katika majadiliano kati ya Marekani na DRC kuhusu madini ? Viongozi hawa waliochaguliwa wana wasiwasi, wanasema, kuhusu kukosekana kwa uwazi kuhusu hali ya upatikanaji wa rasilimali za Kongo, lakini pia kuhusu jinsi utajiri huu utakavyosimamiwa. Wanaonya kuwa bila ya kuwa na dhamana ya wazi, ushirikiano huu unaweza kuzidisha migogoro na rushwa, badala ya kuleta amani na maendeleo.

Nchini DRC, pia, maswali yanaongezeka. Nani anajadili kwa niaba ya nchi? Je, ni ofa gani zinazotolewa kwa Wamarekani? Na chini ya masharti gani? “Tunahitaji kujua matarajio ya serikali katika suala la ofa. Je, ni sehemu gani kuu za ofa hii iliyotolewa kwa Wamarekani kuhusu uchimbaji wa maliasili?” anauliza Jean-Pierre Okenda, mtafiti kuhusu utawala wa madini.

Kwake yeye, ni muhimu sana kuepuka kurudia makosa ya zamani. Anafikiria hasa mkataba maarufu wa China wa mwaka 2008, uliotiwa saini chini ya utawala wa rais Joseph Kabila: madini badala ya miundombinu. “Hatimaye, Kongo ilipoteza Wachina. Hatuna miundombinu leo.” “Jambo la pili tulilopoteza ni kwamba makubaliano hayakuwa na usawa,” anasema.

Hatimaye, maafisa waliochaguliwa wa Marekani wanaomba taarifa rasmi kuhusu mazungumzo yanayoendelea. Wanataka ufafanuzi kuhusu Azimio la Kanuni lililotiwa saini mwezi Aprili kati ya Kinshasa na Kigali chini ya upatanishi wa Marekani, lakini pia kuhusu jinsi masuala ya kibinadamu yatashughulikiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *