DRC: Kusitishwa kwa msaada wa Marekani, uamuzi wenye madhara makubwa

Wakati asilimia 70 ya misaada ya kibinadamu inayotolewa inatoka Marekani, DRC ni mojawapo ya nchi ambapo uamuzi wa hivi majuzi wa Donald Trump wa kusitisha fedha za Marekani kwa ajili ya maendeleo unashuhudiwa kwa ukali zaidi, hasa katika maeneo ya mashariki, ambayo yanakumbwa na vita vikali. Mashirika yasio ya kiserikali nchini Kongo ambayo yanategemea feha hizo, yanasema ni pigo kubwa kwao na shughuli zao zitasimama na itakuwa ngumu sana kukubalika.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa DRC, eneo lialokabiliwa na mzozo mkubwa wa kibinadamu kwa miaka kadhaa sasa, imeshuhudia hali yake ikiwa mbaya zaidi kutokana na mapigano makali yaliyotangulia kukaliwa kwa mji wa Goma na kundi lenye silaha la M23 linaloungwa mkono na Rwanda katika wiki za hivi karibuni. Wakati takriban watu 3,000 wakiwa walifariki, wengi kujeruhiwa na watu 700,000 kuhama makazi yao katika mji mkuu wa Kivu Kaskazini mwezi Januari kulingana na Umoja wa Mataifa, ridadi ya vifo katika eneo hilo ni kubwa.

Lakini mashirika hayo ambayo yanahofia kwamba uharibifu mkubwa sana wa nyenzo pia uliosababishwa na mapigano utafanya kazi yao kuwa ngumu, yanatiwa wasiwasi kwa ukiimarishwa na uamuzi wa Washington, uliochukuliwa Jumatatu Januari 20: hatua ya Donald Trump ya kusimamisha misaada yote ya kimataifa kutoka Marekani. Misaada ambayo, ikiwa na takriban dola bilioni moja, iliwakilisha karibu 70% ya ile iliyolipwa kwa DRC mwaka 2023 na ambayo kusitioshwa kwake ghafla bila shaka kutakuwa na madhara mengi.

“Nina hasira sana, anasema Augustin Karume, mmoja wa viongozi katika shirika moja mjini Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini, eneo ambalo pia limeathiriwa na mapigano makali. 

Ni muhimu sana kwamba msaada wa Marekani udumishwe na kwamba watendaji wa kibinadamu wawe na mwonekano mzuri juu ya kile kitakachotokea, Luc Lamprière mkurugenzi wa Jukwaa la linaloleta pamoja mashirika 124 ya kimataifa yanayofanya kazi nchini DRC