
Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limekanusha siku ya Jumapili Machi 2, 2025 kwamba wapiganaji 20 wanaohusishwa na mauaji ya halaiki nchini Rwanda wanaodaiwa kukamatwa katika ardhi yake, likielezea video ya kukabidhi kwao Rwanda kama “ilitengenezwa”.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Kauli hiyo inakuja baada ya kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda mashariki mwa DRC kusema siku ya Jumamosi limewakamata wapiganaji wa Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kundi la wanamgambo lilioasisiwa na Wahutu walioshiriki katika mauaji ya kimbari ya Watutsi mwaka 1994 nchini Rwanda.
Rwanda kwa muda mrefu imekuwa ikitaja madai ya kuwepo kwa FDLR mashariki mwa DRC ili kuhalalisha uungaji mkono wake kwa M23.
Kwa kuungwa mkono na Rwanda, M23 imeteka maeneo mengi ya mashariki mwa DRC yenye utajiri wa madini na ambayo yanakabiliwa na matatizo katika miezi ya hivi karibuni, ikiwa ni pamoja na miji mikuu ya mikoa ya Goma na Bukavu.
Kundi la M23 lilitoa video inayoonyesha vikosi vyake vikikabidhi washukiwa 20 kutoka kundi la wapiganaji wa FDLR kwa Rwanda kwenye kituo cha mpaka kati ya nchi hizo mbili.
“Hili ni tukio la kubuniwa kwa ladha mbaya iliyopangwa kwa lengo moja tu la kudharau jeshi letu,” imetangaza makao makuu ya jeshi la Kongo katika taarifa.
“Hii ni sehemu ya mkakati wa Rwanda kuhalalisha uvamizi wa baadhi ya maeneo ya eneo la DRC,” makao makuu ya jeshi la Kongo yameongeza.
“Mamlaka ya Rwanda, ambayo ni wataalamu wa sanaa ya uwongo na ghiliba, walichukua wafungwa wa zamani wa FDLR, wakawavisha sare ya jeshi la Kongo na kuwapitisha kama wapiganaji wapya wa FDLR waliokamatwa huko Goma.”
Kamandi kuu ya DRC pia ilishutumu jeshi la Rwanda kwa “mauaji ya kikatili” ya askari waliojeruhiwa na wagonjwa katika hospitali huko Goma, kitendo ambacho “kiinajumuisha uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu,” imesema taarifa hiyo.
Kuongezeka kwa mzozo mashariki mwa DRC kumezusha hofu kwamba huenda ukazidi kuwa vita vya kikanda vinavyohusisha Rwanda, Uganda na nchi nyingine.