
Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Washington iko tayari kujadiliana na Kinshasa makubaliano ambayo Marekani itatoa msaada wa kiusalama kwa DRC ili kupata urahisi wa kupata madini adimu yanayopatikana nchini humo. Ingawa hakuna kilichofanyika bado, majadiliano yanaendelea kati ya nchi hizo mbili.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Ingawa bado ni ya uchunguzi tu, majadiliano kwa lengo la uwezekano wa ushirikiano kuhusu madini adimu ya Kongo kati ya DRC na Marekani yapo rasmi, huku diplomasia ya Marekani ikiwa imethibitisha hili kwa angalau vyombo viwili vya habari – shirika la habari la Reuters na Gazeti la kila siku la Uingereza la Financial Times.
“Marekani iko tayari kujadili ushirikiano katika sekta hii ambao unaendana na ajenda ya utawala wa Trump ‘Marekani Kwanza’,” msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema baada ya seneta wa Kongo kuwasiliana na Washington kupendekeza makubaliano badala ya usaidizi wa usalama.
Soma piaDRC: Misaada ya kibinadamu iko hatarini kutokana na ukosefu wa ufadhili wa kimataifa
Seneta huyo pia alisisitiza kuwa DRC inashikilia “sehemu kubwa ya madini muhimu yanayohitajika kwa teknolojia ya kisasa”, ikiwa ni pamoja na cobalt, coltan na lithiamu, rasilimali zote ambazo uchimbaji wake unakabiliwa na tatizo kubwa: amana nyingi ziko mashariki mwa nchi, eneo ambalo linakabiliwa sasa na mashambulizi makubwa ya AFC/M23 inayoungwa mkono na Rwanda, ambayo mamlaka ya DRC inaishtumu hata hivyo kwa kuchangia kupora na kuchimba kinyume cha sheria madini hayo.
Dhamana za usalama
Ingawa mamlaka ya Kongo haijatoa mapendekezo yao, kwa wakati huu, msemaji wa serikali Patrick Muyaya anahakikisha kwamba maafisa kutoka nchi zote mbili wana majadiliano ya kila siku juu ya suala hili. Mijadala hii iliyoanzishwa na Kinshasa, – ambapo Rais Félix Tshisekedi mwenyewe alionyesha nia yake mwishoni mwa mwezi wa Februari – inaonyesha, kwa vyovyote vile, kwamba DRC imetambua maslahi ya Marekani katika madini na rasilimali za ardhi adimu.
Wazo la ushirikiano unaozidi kuimarika kati ya Marekani na DRC linafanana na lile linalojadiliwa kwa sasa kati ya Washington na Kyiv kwa wazo la kuyapa maslahi ya Marekani upatikanaji wa madini adimu ili kupata dhamana ya usalama.