
Nchini DRC, hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela imeombwa dhidi ya Augustin Matata Ponyo Mapon siku ya Jumatano, Aprili 23, na Mwanasheria Mkuu katika Mahakama ya Kikatiba. Kwa miaka mitatu, kiongozi huyo wa upinzani na Waziri Mkuu wa zamani amefunguliwa mashtaka kwa tuhuma za ubadhirifu wa karibu dola milioni 200 zilizokusudiwa kwa mradi wa Hifadhi ya Chakula ya Bukangalonzo alipokuwa mkuu wa serikali kati ya mwka 2012 na 2016.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kesi hii ilianza kusikilizwa tena kabla ya saa tano saa za DRC. Majaji tisa walikuwepo lakini hakuna mtuhumiwa aliyekuwepo kwa kesi hiyo. Matata Ponyo tayari alikuwa ametangaza kinga yake mpya kama mbunge. Washitakiwa wenzake wawili, gavana wa zamani wa benki kuu Deogratias Mutombo na mfanyabiashara wa Afrika Kusini Christo Grobbler, walitaja sababu za kiafya.
Katika chumba cha mahakama, mvutano umeonekana kuongezeka. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ameimama mbele ya majaji na kutaja mashtaka yanayowakabili washumiwa. “Ni jambo lisilokubalika kuwa mshtakiwa anaweza kuidharau mahakama ya juu zaidi nchini. Kinga si sawa na kutoadhibiwa. Alikuwa chini ya mashitaka alipokuwa mbunge wa taifa. Leo hawezi kutaka kuleta ucheleweshaji na kuzuia mahakama kufanya kazi yake kwa hila na uzushi. “Mshtakiwa huyu anafanya dhihaka na mahakama,” amesema.
Baada ya mapumziko mafupi, hakimu mfawidhi ameamuru kesi iendelee. Wakaguzi wa fedha wamechukua msimamo wa kumshtaki Matata Ponyo, anayetuhumiwa kwa ubadhirifu wa dola milioni 195 katika mradi unaoelezwa kuwa “usioeleweka na uliosimamiwa vibaya.”
Hati ya mashtaka haikuchukua muda mrefu kuwasili: “Vipengele vyote vinavyojumuisha makosa yanayowakabili washtakiwa vimekusanywa, tunaomba mahakama yako iwe radhi kumhukumu kila mmoja wao miaka 20 ya kazi ya kulazimishwa na iamuru wakamatwe mara moja.”
Uamuzi huo utatolewa Mei 14. Upande wa utetezi ulikuwa tayari umepinga mahakama hiyo, ukidai kuwa majaji wawili kati ya hao walikuwa hawastahiki katika kesi hiyo.