DRC: Kampuni ya uchimbaji madini ya China yasitisha shughuli zake Luhwindja kutokana na mapigano

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mapigano yanaendelea kati ya AFC/M23 na Wazalendo katika vijiji kadhaa vya mkoa wa Kivu Kusini, licha ya tangazo la hivi karibuni la kuanza kwa kazi ya uwezekano wa kusitisha mapigano huko Doha, Qatar, na mipango mingine ya kidiplomasia inayoendelea.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kutokana na hali hiyo, kampuni ya uchimbaji madini ya China ya Twangiza Mining imetangaza kusitisha shughuli zake huko Luhwindja katika eneo la Mwenga mkoani Kivu Kusini, kutokana na hali ya usalama kutokuwa shwari katika eneo hilo lenye utajiri mkubwa wa dhahabu.

Katika barua iliyotumwa kwa wafanyakazi wake wote, meneja mkuu wa Twangiza Mining S.A, Chao Xianfeng, ameeleza kuwa kampuni hiyo imelazimika kusitisha shughuli zake huko Luhwindja kwa amri ya utawala mpya uliopo katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.

Mkurugenzi huyo anapendekeza mitambo na magari yote ya Twangiza Mining yaegeshwe katika sehemu tofauti za maegesho kusubiri maelekezo zaidi kutoka kwa uongozi wa juu. Chao Xianfeng pia anapendekeza kupunguza idadi ya wafanyakazi wanaoishi katika kambi mbalimbali za malazi za kampuni ya uchimbaji madini. Hatimaye, anawataka wafanyakazi wasio wakazi “kutoripoti mahali pao pa kazi katika kipindi hiki chote.” “Tutakufahamisha kuhusu maendeleo katika hali hiyo kwa wakati ufaao,” amebainisha.

Hali hii inajiri siku chache baada ya AFC/M23 kuudhibiti mji wa Luhwindja. Kufikia sasa, viongozi wa kundi hilo lenye silaha hawajazungumzia uamuzi huu. Upande wa kusini kidogo, mji wa Uvira bado uko chini ya tishio kutoka kwa waasi. Walionekana mwanzoni mwa juma katikati ya kijiji cha Katogota baada ya mapigano makali na Wazalendo kutoka milima ya Kahamba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *