Muungano wa Common Front for Congo (FCC) wa Joseph Kabila, rais wa zamani wa DRC kinapinga dhidi ya rasimu ya marekebisho ya Katiba iliyowasilishwa na Rais Félix Tshisekedi wiki iliyopita.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jioni ya Jumapili Oktoba 27, muungano wa rais wa zamani umetoa wito wa “kuzuia” mageuzi kupitia “uhamasishaji”. Kambi ya Joseph Kabila pia ilitaka kufanyia marekebisho katiba mwaka 2015, na kuamua kusitisha mradi huo baada ya kupingwa na maandamlano raia na Kanisa.
Nchini DRC, muungano wa Common Front for Congo (FCC) unapinga mpango wa marekebisho ya Katiba na kutoa “wito wa kuhamasisha raia wa Kongo” ili kuzuia mradi huo. Watu “watasimama” “kutetea haki zao”, “uhuru wao”, muungano wa FCC unasema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyochapishwa siku ya Jumapili jioni.

Wiki iliyopita, akiwa Kisangani, Rais Félix Tshisekedi alithibitisha nia yake ya mageuzi hayo na akataja kuanzishwa mwaka 2025 kwa tume maalum ya wataalam.
Martin Fayulu mmoja wa viongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba hakutakuwa na mageuzi au mabadiliko yoyote ya Katiba kabla ya uchaguzi mkuu wa 2028.
Martin Fayulu, ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa mwaka jana, amesema Katiba ya sasa haimzuii mtu yeyote kufanya kazi. Kiongozi huyo wa upinzani ametoa wito kwa raia wa Kongo kuwa tayari kuzuia jaribio lolote la magaeuzi ya katiba.