
Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila anaanza marekebisho ya chama chake cha kisiasa, PPRD. Hatua mpya ilifikiwa siku mbili zilizopita mjini Kinshasa, kwa mkutano wa ofisi ya kisiasa ya chama cha zamani cha rais. Mkutano huo uliongozwa kwa mara ya kwanza na Aubin Minaku, naibu kiongozi mteule wa PPRD na sasa anakaimu kama rais wa mpito wa chama hicho. Maamuzi muhimu yamechukuliwa ili kufufua shughuli za chama.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Nchini DRC, uamuzi wa kwanza uliotangazwa unahusu kuundwa kwa kitengo cha uchambuzi na utabiri. Chombo hiki kitaambatanishwa na ofisi ya kisiasa na sekretarieti ya kudumu ya chama. “Lazima tuweze kutathmini dhana zote zinazowezekana kuhusu maendeleo ya nchi,” Aubin Minaku amemwambia Patient Ligodi mwandishi wa timu ya wahariri ya kitengo cha RFI kanda ya Afrika. Kulingana na Aubin Minaku , itakuwa aina ya maabara ya mawazo. Seli hii, iliyofafanuliwa kama ya kimkakati, itaundwa ndani ya siku kumi, na uteuzi wa viongozi wake ndani ya muda kama huo.
Uteuzi zaidi unatarajiwa, ikijumuisha nafasi nne kati ya sita zilizo wazi za naibu katibu mkuu. Mabadiliko pia yanapangwa katika ngazi ya mkoa, kwa nia ya kupanga upya chama. Marekebisho haya pia yanalenga uchaguzi mkuu wa mwaka 2028.
Aubin Minaku anaeleza kuwa chama hicho kinajiona kuwa katika upinzani dhidi ya kile inachokiita udikteta. Ili kubeba kasi hii mpya, kitengo cha mawasiliano cha chama hicho pia kitapangwa upya na kitaalamu, huku kikiimarika ndani na nje ya nchi.
Joseph Kabila, kwa upande wake, bado hayupo nchini. “Yuko nje ya nchi kwa ajili ya mradi wake wa udaktari. Lakini pia kwa sababu za kiusalama. Kabla ya kuondoka kwake, alikuwa akikabiliwa na dhuluma za kisiasa na vitisho,” anaeleza Aubin Minaku. Akiulizwa kuhusu kurudi kwa Joseph Kabila nchini DRC, ” Aubin Minaku amesema kiongozi wake yuko tayari kurundi lakini dhamana za usalama zinahitajika,” anasisitiza Aubin Minaku.