DRC: Joseph Kabila ametembelea Mji wa Goma mashariki ya DRC

Rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila ametembelea Mji Mkuu wa Kivu Kaskazini  Goma mashariki mwa DRC baada yake kurejea nchini humo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Habari za kuwasili kwake zilithibitishwa kwa RFI mnamo Ijumaa, Aprili 18, na vyanzo viwili vya karibu na AFC/M23 na chanzo kutoka kwa msafara wa mkuu wa zamani wa nchi.

Kulingana nao, Joseph Kabila alipitia Kigali kabla ya kufika mji mkuu wa Kivu Kaskazini.

Vyanazo vya taarifa hii  vikiwemo M23 na maofisa wa usalama nchini Rwanda aidha vinaeleza kwamba kiongozi huyo wa zamani aliwasili Goma Ijumaa ya wiki hii akitokea katika eneo la mpaka wa Gisenyi kati ya Goma na Rwanda.

Licha ya kuwasili kwa Kabila, yeye mwenyewe hajaonekana hadharani wala kutoa taarifa kuthibitisha kuwasili kwake nchini DRC.

Rais wa DRC mara kwa mara amekuwa akisema mtangulizi wake anashirikiana na waasi wa M23
Rais wa DRC mara kwa mara amekuwa akisema mtangulizi wake anashirikiana na waasi wa M23 © JOSPIN MWISHA / AFP

Hatua ya kuwasili kwa Kabila imezua mjadala makali mashariki mwa DRC, baadhi wakiwa na matumaini na wengine wasiwasi ya hali ya kiusalama kuendelea kuwa mbaya haswa baada ya rais Tshisekedi kumtuhumu mtangulizi wake kwa kushirikiana na waasi wa AFC/M23.

Maswali mengi ambayo yanaibuliwa na wakazi wa Goma ni kwamba kwa sasa yuko wapi Joseph Kabila baada yake kuutembelea Mji huo wa Goma? Bado angali katika Mji huo au ameondoka tena kurejea Rwanda alipotokea?

Wengine wanauiliza ni kwa nini Kabila ameibukia tena haswa wakati huu ambao mzozo kati ya DRC na Rwanda unaonekana kushika kasi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *