
Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Ulaya katika kanda ya Maziwa Makuu, Johan Borgstam, aanazuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanzia tarehe 2 hadi 5 Machi kama sehemu ya uungaji mkono wa Umoja wa Ulaya kwa juhudi za amani za kikanda.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Johan Borgstam alikutana na Rais Félix Tshisekedi Jumanne, Machi 4, ikiwa ni ziara yake ya nne katika eneo hilo katika muda wa miezi sita. Siku ya Jumatano mjini Kinshasa, Johan Borgstam amesisitiza tena msimamo wa Umoja wa Ulaya kuhusu mzozo unaotikisa eneo hilo.
Umoja wa Ulaya unakataa shtaka lolote la viwango viwili vya uchokozi. Huu ndio ujumbe ambao Johan Borgstam anadai kuwa alimwambia Rais wa Rwanda Paul Kagame wakati wa mkutano wao wiki moja iliyopita. Jibu kwa ukosoaji wa kulinganisha msimamo wa Umoja wa Ulaya juu ya vita vya Ukraine na uwepo wa Rwanda nchini DRC, kulingana na ripoti za Umoja wa Mataifa. Mjumbe maalum wa Umoja wa Ulaya anasisitiza: “Kuheshimu sheria za kimataifa lazima iwe kipaumbele kila mahali duniani. “
Kuhusu suala la vikwazo, Brussels inaenda kwa kasi yake yenyewe. Mnamo tarehe 24 Februari, alisema, Nchi Wanachama zilichukua uamuzi wa kisiasa: kuendelea kuandaa orodha ya vikwazo vitakavyolenga baadhi ya viongozi nchini Rwanda. Sasa, mawakili wa Ulaya ndio wanaochunguza faili hizo ili kuhakikisha kwamba tuhuma hizo ni za msingi na zinazingatia sheria za Ulaya.
Tofauti na vikwazo vya Umoja wa Mataifa au Marekani, vile vya Umoja wa Ulaya vinahitaji mchakato wa kisheria wa wiki mbili hadi tatu kabla ya kupitishwa kwa mara ya mwisho, anabainisha Nicolas Berlanga Martinez, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini DRC.
Upatikanaji wa uwanja wa ndege wa Goma,mada nyeti
Suala jingine nyeti ni lile la kufikia uwanja wa ndege wa Goma, ulio chini ya udhibiti wa AFC/M23. Johan Borgstam anadai pia kuzungumzia suala hili kwa mamlaka ya Rwanda. “Sio serikali ya Kongo wala MONUSCO inayodhibiti eneo hilo,” anasema mwanadiplomasia huyu wa Ulaya.
Hali hii inazuia operesheni yoyote ya kibinadamu au ya vifaa kuelekea mashariki mwa nchi. Hakuna suluhisho lkuhuu masuala ya anga linalowezekana katika hatua hii, anaelezea Johan Borgstam. Njia pekee ya kufika Goma inasalia kuwa njia ya kupitia Nairobi, ikifuatiwa na msafara wa lagari yakitumia njia ya ardhini.