
Nchini DRC, Constant Mutamba, Waziri wa Sheria, amepingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Mahakama ya Juu, Firmin Mvonde, jana, Jumanne, Juni 10, katika barua ambayo RFI imepata kopi. Uamuzi huu unakuja siku moja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuliomba Bunge kuidhinisha kufunguliwa mashtaka kwa Waziri wa Sheria.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi
Constant Mutamba anakabiliwa na kesi ya ubadhirifu. Bado kuna utata kuhusu utoaji wa kandarasi ya umma ya dola milioni 29 kwa kampuni iliyopewa jukumu la kujenga jela huko Kisangani, katika mkoa wa Tshopo. Kati ya fedha hizo, dola milioni 19 zilidaiwa kutolewa bila kufuata taratibu za manunuzi. Kulingana na upande wa mashtaka, fedha hizi hazitoki katika hazina ya umma, bali kwenye Mfuko wa Fidia na malipo kwa Wahasiriwa wa Shughuli Haramu za Uganda nchini DRC (Frivao). Shirika hili lililo chini ya usimamizi wa Wizara ya Sheria. Kwa hivyo ilitokaje kwenye mfuko uliokusudiwa wahasiriwa kwenda kwa tuhuma za ubadhirifu?
Awamu tano za dola milioni 65
Mnamo mwaka 2022, Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliamuru Uganda kulipa dola milioni 325 kwa DRC. Uamuzi huu ulifanywa kama fidia kwa unyanyasaji uliofanywa kati ya mwaka 1998 na 2003 katika eneo la mashariki mwa nchi. Malipo hayo yamepangwa kufanywa kwa awamu tano za dola milioni 65. Hadi sasa, malipo matatu yamefanywa, jumla ya dola milioni 195. Pesa hizi hutumiwa kufadhili Frivao, Mfuko maalum inayokusudiwa kuwafidia wahasiriwa. Mfuko huu ungeliaanza kufanya kazi kikamilifu mnamo mwaka 2023.
Alipowasili katika wizara hiyo, Constant Mutamba alishutumu kutofanya kazi vizuri, “kutoendana,” alisema, “kati ya kiasi kilichotolewa na hatua zilizotekelezwa.” Ofisi yake ilibainisha kuwa chini ya timu ya awali, waathirika zaidi ya mia moja walilipwa fidia katika mwaka mmoja. Lakini tangu Agosti 2024, malipo yameanza tena. Kiasi kinacholipwa kwa kila mtu kimeongezeka kutoka dola 200 hadi dola 2,000. Na, katika miezi minane, zaidi ya wahasiriwa 14,000 wamelipwa fidia, kulingana na Frivao.
Ripoti ya bunge pia inaonyesha kwamba Ukaguzi Mkuu wa Fedha unadaiwa kumpa waziri fomula ya ugawaji: 12% ya fedha zimetengwa kwa Wizara ya Sheria. Kulingana na Constant Mutamba, hisa hii inatumika kufadhili miradi mingine ya umma katika eneo la Mashariki Zaidi. Hivyo, waziri anakataa tuhuma zozote za matumizi mabaya ya fedha. Anazungumzia “vita” na “njama ya kisiasa.” Katika barua ambayo RFI ilipata kopi, alitangaza kuwa anapingana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na mahakimu walio chini ya mamlaka yake.