DRC: Chama cha Joseph Kabila chapinga kuitishwa kwa maafisa wake mahakamani

Maafisa wa chama cha PPRD, chama cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila Kabange, wameitishwa mbele ya mahakama za kijeshi. Naibu kiongozi wa chama hicho Aubin Minaku, katibu mkuu Ramazani Shadary, naibu wake Ferdinand Kambere na maafisa wengine kumi na wawili wakuu wa chama hicho walitarajiwa asubuhi ya leo mbele ya ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi wa Kinshasa-Gombe.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Katika vibali hivyo vya kuitishwa, hakuna sababu iliyotolewa. Wote wameitwa “kutoa mwanga mbele ya mahakama.” Mamlaka zinamshutumu rais huyo wa zamani kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 walioteka miji ya Goma na Bukavu mashariki mwa DRC mwezi Januari na Februari. Chama cha PPRD, kinasema “huu ni uthibitisho wa udikteta” .

“Sisi ni Warepublican”

“Tunashangaa kuona tunaanza kualikwa ili tutoe taarifa za uwezekano wa kushirikiana na vuguvugu la uasi tusilolijua na ambalo mamlaka zinafahamu kuliko sisi. Sisi ni Warepublican, tunaheshimu taasisi za Jamhuri. “Wakongo wanajua kuwa PPRD ndicho chama kikuu cha upinzani,” amesema François Nzekuye wa PPRD kabla ya mkutano huo.

“Utawala wa Tshisekedi unatafuta kuangushia makosa watu wasio na hatia”

“Sisi tuko watulivu na watu wa Kongo wanatambua siku hadi siku kwamba mamlaka ya utawala wa Tshisekedi inatafuta kuangushia makosa watu wasio na hatia na wananchi wanajua. Tulilifanya jeshi la Kongo kuwa jeshi la 11 lenye nguvu barani Afrika. Watumishi wa serikali na wafanyakazi walilipwa mara kwa mara. Haya yote yanakuwa ndoto isiyoweza kuelezeka kwa mamlaka hii ambayo haijui jinsi ya kusimamia au kushughulikia mahitaji ya raia. “

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *