
Mwanzilishi mwenza wa Mkataba wa Kijamii wa Amani na Kuishi Vizuri pamoja nchini DRC ili kumaliza mzozo unaosambaratisha Mashariki mwa nchi hiyo, Baraza la Maaskofu wa Kitaifa wa Kongo (CENCO) limefanya mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa hii, Mei 16, ambapo limeomba kutekelezwa kwa mradi linalotetea na Kanisa la Kiprotestanti nchini DRC.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Paulina Zidi
Likishirikiana na Kanisa la Kiprotestanti la Kongo katika rasimu ya Mkataba wa Kijamii wa Amani na Kuishi Vizuri pamoja nchini DRC, Kanisa Katoliki la Kongo kwa mara nyingine tena limesisitiza haja ya kupata muafaka wa kurejesha utulivu wa kikatiba na kuboresha maridhian kati ya Wakongo siku ya Ijumaa, Mei 16. Kutokana na tathmini isiyo na maelewano ambayo linaifanya kuzungumzia kuhusu hali nchini humo, hususan vita na migogoro inayozidi kukuwa, mzozo wa kisiasa unaoendelea kuongezeka. baraza hili pia linabaini kwamba mpango linaotetea ni muhimu zaidi kuliko mambo mengine.
Kufuatia wiki kadhaa za mashauriano ya pamoja na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) nchini DRC, lakini pia katika eneo hilo na hata Ulaya, Marekani na Qatar, Baraza la Maaskofu wa Kitaifa la Kongo (CENCO) pia linapenda kutangaza kwamba ripoti iliyoandikwa iko tayari.
Ingawa mkutano wa kwanza umetengwa kwa mkuu wa nchi, Félix Tshisekedi, kwa sababu “hatutaweza kusonga mbele bila makubaliano yake,” kulingana na Donatien Nshole, katibu wa CENCO, mkutano huo wa mwisho unasisitiza haja ya kuandaa kongamano la kitaifa kushughulikia sababu kuu za mzozo mashariki mwa nchi na kutafuta mwafaka wa ndani. “Bila haya, bado kutakuwa na makundi yenye silaha,” anaonya, akiongeza kuwa “jukwaa hili lazima lisiwe nafasi rahisi ya kugawana madaraka.”
Mara tu mwafaka utakapofikiwa, kongamano hili linaweza, katika awamu ya pili, kusababisha kuandaliwa kwa mkutano mkuu wa kimataifa kuhusu Maziwa Makuu ambapo Rais Tshisekedi angezungumza kwa niaba ya raia wa Kongo, anaongeza Askofu Nshole. “Tena, hili ni jibu kwa wale wanaoamini kuwa huu ni mpango wa kumpindua mkuu wa nchi: hapana! “Yeye ndiye atakayeongoza katika mazungumzo katika mkutano huu,” anasisitiza askofu huyo, ambaye anasema mkutano mpya na Félix Tshisekedi unapaswa kufanyika haraka sana.