DRC: Bunge laidhinisha Waziri wa Sheria Constant Mutamba kufunguliwa mashitaka

Bunge la taifanchini DRC limeidhinisha Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Juu jioni ya Jumapili, Juni 15, kumfungulia mashitaka Constant Mutamba, Waziri wa Sheria wa DRC. Anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma kuhusiana na mradi wa ujenzi wa gereza huko Kisangani, kaskazini mashariki mwa nchi, na kwa hivyo anapaswa kujiuzulu wadhifa wake kwa mujibu wa sheria.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchini DRC, wabunge wamefanya uamuzi wao katika kikao cha faragha. Kati ya wabunge 363 waliopo, 329 wamepiga kura ya kuunga mkono kumshtaki Waziri wa Sheria Constant Mutamba. Idhi hii ya bunge inafungua njia ya kuanzishwa kwa kesi katika siku zijazo. Kuhusu waziri anayetuhumiwa, anatarajiwa kujiuzulu, kama inavyotakiwa na sheria, mapema wiki hii.

Constant Mutamba, 37, anatuhumiwa kuhamisha dola milioni 19 kwa kampuni ya kibinafsi kama sehemu ya kandarasi ya kibinafsi ya ujenzi wa gereza huko Kisangani. Mkataba huo ulikuwa wa thamani ya dola milioni 29, 65% ambazo zilikuwa zimelipwa tu, ingawa sheria ya manunuzi ya umma inaweka kikomo cha malipo ya awali hadi 30%. Mkataba huo haukuwa umeidhinishwa na Waziri Mkuu.

Kampuni hewa

Wabunge na mwendesha mashtaka wanaamini kwamba kiasi hiki kingeweza kufujwa ikiwa kitengo cha taifa cha kijasusi cha kifedha hakingezuia akaunti ya walengwa kwa wakati na kutoa tahadhari.

Kampuni inayozungumziwa inaelezewa haijawahi kuwepo na haina ofisi inayojulikana, haina wafanyakazi. Ripoti iliyoidhinishwa na wabunge hao pia inaeleza kuwa eneo ambalo kazi hiyo ingefanywa haipo.

Wasaidizi wa Waziri wanashtumu unyanyasaji usiokoma

Kwa walio karibu na Waziri, kwa vile fedha hizo hazikupokelewa na kampuni, hakuna suala la ubadhirifu. Wasaidizi wa Waziri wa Sheria pia wanachukulia waziri huyo ni mwathirika wa “mageuzi yake ya mahakama na mitandao ya kimafia ambayo imesambaratishwa.”

Hata hivyo Bunge pia lilikataa kuchunguza shtaka la pili la mwendesha mashtaka dhidi ya waziri huyo, linalohusiana na mashtaka ya kudharau mahakama na “uchochezi wa kuvunja mamlaka ya umma.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *