
Kamati ya fedha ya Bunge la taifa inachunguza kwa karibu bajeti ya juhudi kutoa motisha kwa wanajeshi walio vitani. kamati hiyo imeanza mfululizo wa vikao na wajumbe wa serikali ili kuthibitisha kuwa sekta ya ulinzi na usalama ina rasilimali zinazohitajika. Baada ya kusikilizwa kwa Naibu Waziri Mkuu anayesimamia Utumishi wa Umma, Jean-Pierre Lihau, viongozi wengine wakuu watasikilizwa wiki hii. Je, mpango huu una upeo gani?
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi
Kazi hii ya uuchunguzi ni sehemu ya muktadha ambapo matumizi ya usalama na misaada ya kibinadamu yameongezeka sana, kutoka 3% ya bajeti ya taifa mwaka wa 2021 hadi 22% mwaka wa 2023. Suala hili ni muhimu zaidi kutokana na kwamba mpango wa serikali wa miaka mitano, uliowasilishwa mwaka wa 2024, hutoa kitita cha dola zaidi ya bilioni 18, kwa ulinzi na usalama sawa na 20% ya bajeti ya jumla.
Ufanisi wa jeshi watiliwa shaka
Hata hivyo, ufanisi wa jeshi la Kongo kufuatia kusonga mbele kwa vuguvugu la kisiasa la AFC/M23 – linaloungwa mkono na Rwanda – unaendelea kutiliwa shaka, huku wengine bado wakiashiria ukosefu wa uwezo. Ni kwa msingi wa angalizo hili kwamba Kamati ya Uchumi na Fedha ya Baraza la Wawakilishi imeanzisha operesheni hii. Lengo ni kutoa majibu sahihi kwa maswali kadhaa muhimu.
Je, serikali inahitaji kiasi gani kuunga mkono juhudi za vita? Ni malengo gani yanapaswa kufikiwa? Jinsi ya kuhakikisha usimamizi mzuri na wa uwazi wa fedha? Ni lazima kusema kwamba mada inasubiri kujadiliwa na serikali. Tangu mwisho wa mwezi wa Januari 2025, Baraza la Mawaziri limekuwa likizingatia suala hilo na tayari limepitisha ripoti inayofafanua masharti ya kuongeza mishahara na marupurupu ya wanajeshi na polisi.
Mishahara ya kijeshi kuongezeka maradufu
Hatua zilizotangazwa ni pamoja na kuongeza maradufu mshahara wa wanajeshi na kuanzisha bonasi maalum ya mapigano mara moja. Katika hali hii, Tume ya Uchumi na Fedha ya Bunge la taifa la DRC itaendelea na kazi yake ya kusikiliza wajumbe kadhaa wakuu wa serikali: Naibu Waziri Mkuu anayeshughulikia Mambo ya Ndani na Usalama, Waziri wa Bajeti na pia Gavana wa Benki Kuu.