Corneille Nangaa, mratibu wa AFC/M23, vuguvugu la kisiasa na kijeshi linaloungwa mkono na Kigali, aliwasili Bukavu, mji mkuu wa Kivu Kusini siku ya Jumanne, Februari 25,, siku kumi baada ya kundi lake kuudhibiti mji huo. Kusonga mbele huku kunaashiria hatua mpya katika maendeleo ya AFC/M23, ambayo inaonekana kuendelea na njia yake kuelekea kusini.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Tangu mwisho wa mwezi wa Januari, AFC/M23, inayoungwa mkono na jeshi la Rwanda, imepata mafanikio makubwa kwa mkoa wa kuvuka Kivu Kusini. Kundi hilo kwanza liliteka Minova, kitovu kikuu cha biashara kaskazini mwa mkoa huo, kabla ya kuendelea kilomita 150 kwa mwezi mmoja, kufika Bukavu. Japokuwa kulikuwa na mashambulizi ya anga ya jeshi la anga la Kongo au vikosi vya Burundi havikuzuia kusonga mbele kwa wapiganaji wa kundi hili.
Waasi wa AFC/M23 walichukua udhibiti wa eneo moja karibu na Kamanyola, lililoko kilomita 45 kusini mwa Bukavu. Katika eneo hili kunapatikana sehemu muhimu ya kijeshi la FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo), sehemu ambayo ilichukuliwa na kundi hili la waasi. Kilomita 40 tu kutoka Uvira, AFC/M23 inakaribia mji wa pili wa Kivu Kusini, kufuatia eneo linaloweza kufungua njia ya kwenda katika mko wa Tanganyika.
Hali ya wasiwasi yatanda Uvira
Huku vuguvugu la kisiasa na kijeshi likiendelea, Uvira ilikumbwa wiki iliyopita na machafuko. Kuliriptiwa visa vya uporaji, wanamgambo wa ndani na baadhi ya wanajeshi wa Kongo wananyooshewa kidole kuhusika na vitendo hivyo. Ukosefu huu wa usalama umesababisha watu wengi kutoroka makazi yao: wakaazi wengi wa mji huo wamekimbilia Burundi na Tanzania, wakati wengine wanachukua barabara kuelekea Kalemie, mji mkuu wa mko wa Tanganyika, ambayo inaweza kuwa lengo linalofuata la kundi hili la waasi. Tangu wakati huo, mamlaka imekuwa ikijaribu kurejesha udhibiti. Jean-Jacques Purusi, gavana wa mko wa Kivu Kusini, alipokelewa siku ya Jumatano mjini Kinshasa na Félix Tshisekedi. Alisema amepokea maagizo kutoka kwa mkuu wa nchi ya Kongo kusimamia mkoa huo kutoka mji wa Uvira.
Burundi inadumisha uwepo wake kuzuia AFC/M23
Wanajeshi wa Burundi wanaendelea kutumwa mashariki mwa DRC, licha ya uvumi kuwa wako wanondoka na kurejea nchini mwao. Wanajeshi wa Burundi waliotumwa kusaidia FARDC kuzuia AFC/M23, kusonga mbele bado wanaripotiwa kwenye barabara kadhaa, kulingana na shuhuda nyingi.
Vikosi vya Burundi vipo kwenye Barabara ya taifa Nambari 5, haswa kwenye mhimili wa Luvungi-Uvira, kilomita 10 tu kutoka ngome za AFC/M23, kulingana na mashahidi. Baadhi ya vitengo vinasemekana kurejea kutoka Bukavu, mji uliangukia mikononi mwa kundi hilo la waasi mnamo Februari 14, huku vingine vikitumwa moja kwa moja kutoka Burundi. Idadi yao kamili bado haijajulikana katika hatua hii, lakini lengo liko wazi: kuzuia Uvira, mji ulioko katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, usianguke mikononi mwa wapiganaji wa AFC/M23, kulingana na chanzo cha kijeshi.
Mjini Bujumbura, maendeleo haya yanafuatiliwa kwa karibu. Burundi inahofia kuona AFC/M23, inayoungwa mkono na Rwanda, kuweka kambi kwenye milango ya mji mkuu wake wa kiuchumi. Uhusiano kati ya Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame umezorota sana katika miezi ya hivi karibuni, na rais huyo wa Burundi anamshutumu waziwazi jirani yake wa Rwanda kwa kutaka kuhatarisha usalama wa nchi yake.
Ikiwa Uvira itaaanguka mikononi mwa waasi wa AFC/M23, itafungua njia kuelekea Tanganyika
Kwa nini mko wa Tanganyika ni muhimu? Ni sehemu ya eneo la Katanga, injini ya kiuchumi ya DRC. Tajiri wa rasilimali muhimu za madini (cassiterite, dhahabu, koltani, zumaridi, fedha, shaba, nikeli), pia hufungua njia kwa mikoa mingine ya Katanga ya zamani, ambao yote pia tajiri kwa madini. Kwa kufahamu masuala haya, mkuu mpya wa majeshi ya FARDC, Luteni-Jenerali Banza Mwilambwe, ameichagua Kalemie kwa misheni yake ya kwanza tangu kuteuliwa kwake mwezi Desemba 2024. Ujumbe wake uko wazi: kudumisha nidhamu katika safu, kulinda raia na kuzuia AFC/M23 kufikia mkoa huu wa kimkakati.
