
Rais wa Marekani ametangaza Jumatano, Februari 12, kwamba alikuwa na “mazungumzo ya muda mrefu na yenye tija” na mwenzake wa Urusi. Donald Trump na Vladimir Putin wamekubaliana “kufanya kazi pamoja, kwa karibu sana” na kuanza mazungumzo “mara moja” kuhusu Ukraine. Kremlin inabainisha kwamba inataka “suluhisho la muda mrefu” la mzozo wa Ukraine kupitia “mazungumzo ya amani”. Marais hao wawili wanapanga kukutana kwa mara ya kwanza nchini Saudi Arabia.
Imechapishwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
Mazungumzo ya simu kati ya Donald Trump na Vladimir Putin sikuya Jumatano, Februari 12, yalikuwa na matunda, kulingana na kauli ya rais Donald Trump kwenye mtandao wake wa Truth Social. “Tumekubaliana kufanya kazi pamoja, kwa ukaribu sana, ikiwa ni pamoja na kutembeleana katika nchi zetu,” rais wa Marekani ameeleza. Kremlin inabainisha kwamba Washington na Moscow zimekubali “kufanya kazi pamoja.”
Donald Trump anaeleza kwamba amekubaliana na mwenzake wa Urusi kuanza mazungumzo “mara moja” kuhusu Ukraine. Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov amewaambia waandishi wa habari kwamba Vladimir Putin amemwambia rais wa Marekani kwamba anataka kupata “suluhisho la muda mrefu” la mzozo wa Ukraine kupitia “mazungumzo ya amani.” “Rais Putin ametaja haja ya kushughulikia vyanzo vya mzozo huo,” amesema.
Trump na Putin kukutana Saudi Arabia
Uhusiano huu wa moja kwa moja kati ya nchi hizi mbili ni mbali na vitendo. Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alikuwa hajazungumza na Vladimir Putin kwa zaidi ya miaka mitatu na alikuwa ameanzisha vikwazo vingi dhidi yake, anakumbusha mwandishi wa RFI nchini Marekani, David Thomson.
“Tunataka kukomesha mamilioni ya vifo vinavyohusishwa na vita vya Urusi na Ukraine. Rais Putin hata ametumia kauli mbiu yangu ya kampeni: “AKILI YA KAWAIDA.” “Sote wawili tunaiamini sana,” amesema rais wa Marekani, ambaye kisha amezunumza na rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, kujadili mazungumzo yake na mkuu wa Kremlin.
Kulingana na Dmitry Peskov, Vladimir Putin “amemwalika Donald Trump kutembelea Moscow na akaelezea utayari wake wa kupokea maafisa wa Marekani nchini Urusi.” Na wote wawili “walikubali kuendelea na mawasiliano ya kibinafsi, ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya ana kwa ana.”
Ziara ya mwisho ya rais wa Marekani nchini Urusi ilikuwa mwaka 2013, David Thomson anasema. Saa chache baada ya ujumbe wake wa kwanza kwenye mtandao wake wa Truth Social, rais huyo wa Marekani amewaambia waandishi wa habari kutoka Ikulu ya Marekani kwamba yeye na Vladimir Putin watakutana hivi karibuni nchini Saudi Arabia, bila kutaja tarehe. “Hatimaye tutakuwa na usitishaji mapigano katika siku zijazo na sio mbali sana,” ameongeza.
Ishara mbaya kwa Kyiv
“Tumezungumza juu ya nguvu za mataifa yetu na faida kubwa ambayo siku moja itakuja kutokana na kufanya kazi pamoja,” ameandika Donald Trump, ambaye ametaka “kumshukuru Rais Putin kwa muda na jitihada alizotoa kwa mazungumzo haya a simu, na kwa kuachiliwa kwa Marc Fogel” siku ya Jumanne, Februari 11 baada ya kuzuiliwa miaka mitatu nchini Urusi. Siku ya Jumatano, Februari 12, Marekani ilikubali kumwachilia mtaalam wa IT wa Kirusi Alexander Vinnik, anayeshutumiwa kwa uhalifu unaohusiana na jukwaa la kubadilishana fadhaa la BTC-e.
Mbali na mwanzo huu wa ukarabati wa Vladimir Putin kwenye anga ya kimataifa ambayo inaonekana iko mezani, mazungumzo ya nchi mbili kati ya Urusi na Marekani ndio hali ambayo Ukraine ilitaka kuepukwa, anabainisha Emmanuelle Chaze, mwandishi wa RFI huko Kyiv. “Hakuna mazungumzo juu ya Ukraine bila Ukraine” imekuwa kauli mbiu ya washirika wa Ukraine hadi sasa; Mazungumzo kati ya Washington na Moscow bila Volodymyr Zelensky yangetuma ishara ya wazi kutoka kwa Marekani, ambayo iko katika mchakato wa kupatana na Urusi.
Zelensky anaamini katika ‘nguvu ya Marekani’ ‘kupata njia ya amani’
Kauli za Donald Trump kutoka Ofisi ya Oval pia sio za kutia moyo sana kwa viongozi wa Ukraine. Rais amesema kwamba “itabidi kuwe na uchaguzi wakati fulani” nchini Ukraine na kwamba uanachama wa Ukraine katika NATO “haukuwa wa kweli.”
Volodymyr Zelensky hata hivyo ametuma ujumbe wa matumaini kwa taifa la UkRaine, akizungumzia “mazungumzo mazuri” na rais wa Marekani: “Ninashukuru kwa nia ya dhati ya rais wa Marekani katika fursa hii ya pamoja na jinsi tunaweza kufikia amani pamoja. Mazungumzo yalikuwa marefu, na tumejadili mambo kadhaa, kijeshi, kiuchumi…