Donald Trump na Cyril Ramaphosa wajibizana vikali katrika mazungumzo yao White House

Ulikuwa ni mkutano uliotarajiwa kwa kiasi kikubwa, huku kukiwa na wasiwasi kutokana na uhusiano mbaya kati ya Afrika Kusini na Marekani tangu kurejea kwa Donald Trump katika Ikulu ya White House. 

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani amempokea mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, katika Ofisi ya Oval ya White House siku ya Jumatano, Mei 21. Rais wa Afrika Kusini amehakikisha kwamba mkutano huo umekwenda “vizuri sana” na akasema anatarajia Donald Trump kuhudhuria mkutano wa G20 huko Johannesburg mnamo mwezi Novemba.

Wawili hao wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu walichosema, lakini mazungumzo yaliendelea kuwa mazuri na yenye heshima. Mvutano huo ulikuwa dhahiri, lakini mambo haya kuwa mabaya zaidi kama ilivyoshuhudiwa wakati wa alipopokelewa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mnamo mwezi wa Februari 2025. Na hata hivyo, Ikulu ya White House ilikuwa imetayarisha mambo yake, kwani baada ya hapo Donald Trump amerusha picha za mikutano ya hadhara ambapo viongozi wa kisiasa walitaka kuuawa kwa watu weupe, na picha zingine maeneo yenye dalili ya misalaba ambayo Donald Trump alisema ni makaburi ya wakulima wazungu.

“Kuna watu wengi wanaohisi kuteswa na wanaokuja Marekani,” Donald Trump ambainisha. Tunachukua sehemu nyingi, ikiwa tunahisi kuna mateso au mauaji ya kimbari. Tuna watu wengi, lazima nikwambie Mheshimiwa Rais, kwa ujumla wakulima wazungu wanakimbia Afrika Kusini.”

Cyril Ramaphosa ameeleza kuwa harakati za kisiasa zinazoonyeshwa kwenye video hizi si sehemu ya muungano wake na kwamba sio sera ya Afrika Kusini kutekeleza wito huu wa chuki. Anahakikisha kuwa hapana, hakuna unyakuzi wa ardhi ya kilimo bila fidia nchini Afŕika Kusini. Hatimaye, yeye na ujumbe wake walimweleza Donald Trump kwamba nchi hiyo inakabiliwa na tatizo la uhalifu ambalo kwa hakika linawaathiri wakulima weupe, lakini hilo ni la jumla na linagharimu maisha zaidi ya watu weusi na alimwomba Donald Trump msaada wa Marekani ili kupambana na uhalifu huu uliokithiri kwa njia za kiteknolojia na kwa njia za kiuchumi kupitia ushirikiano mpya.

Cyril Ramaphosa alikuja na wajumbe wa aina mbalimbali, hasa katika masuala ya rangi ya ngozi. Hasa, Waziri wake wa Kilimo, John Steenhuisen, ambaye, kama jina lake linavyoonyesha, ni kutoka jamii ya afrikaners, watu wachache wanaodaiwa kuteswa nchini kwa mujibu wa utawala wa Marekani. Ametetea sera ya kilimo ya Afrika Kusini.

“Rais Trump anapaswa kuwasikiliza Waafrika Kusini, ambao baadhi yao ni marafiki zake wazuri, kama wale wa hapa. “Ningesema kwamba kama kungekuwa na mauaji ya halaiki ya wakulima wa afrikaners, ninaamini kwamba waungwana hawa hawangekuwa hapa,” Cyril Ramaphosa amesema.

Na kisha rais wa Afrika Kusini alijua jinsi ya kumlainisha mwenzake kupitia hisia zake kwa namna anavyopenda mchezo wa gofu, kwa kuandamana katika ujumbe wake na wachezaji wawili wakubwa wa Afrika Kusini wa gofu, Ernie Els na Retief Goosen, ambao walikuwa na zawadi ya kumlainisha Donald Trump na kuruhusu mkutano kumalizika kistaarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *