Donald Trump: Marekani na Iran ziko kwenye majadiliano ‘ya moja kwa moja’ kuhusu suala la nyuklia

Wakati Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu akifanya ziara nyingine katika Ikulu ya White House siku ya Jumatatu, Aprili 7, rais wa Marekani ametangaza kuwa Washington imefungua mazungumzo “ya moja kwa moja” na Tehran kujadili suala la nyuklia. Baadaye kidogo, mkuu wa diplomasia ya Iran amebaini kufanyika kwa mazungumzo “yasiyo ya moja kwa moja” siku ya Jumamosi, Aprili 12, huko Oman.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Wakati Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran zimekuwa hazina uhusiano wowote wa kidiplomasia tangu mwaka 1980 na Donald Trump kuiondoa nchi yake katika makubaliano ya nyuklia ya Iran yaliyojadiliwa na Barack Obama katika muhula wake wa kwanza, rais wa Marekani hata hivyo anasisitiza kuwa nchi yake iko katika mazungumzo ya moja kwa moja na Iran.

“Tuna majadiliano ya moja kwa moja na Iran. Yameanza na yataendelea Jumamosi [Aprili 12] kwa mkutano mkubwa sana na tutaona kitakachotokea. Nadhani kila mtu atakubali kwamba kufikia makubaliano itakuwa vyema kuliko njia mbadala iliyo wazi. Na kwamba mbadala wa wazi sio mahali ninapotaka kwenda au kusema ukweli ambapo Israeli inataka kwenda ikiwa inaweza kuiepuka. “Kwa hivyo tutaenda kuona ikiwa tunaweza kuipepuka”, amesema Trump ambaye pia amesema kuwa Iran itakuwa katika hatari kubwa iwapo mazungumzo hayo hayatafanikiwa.

Tehran inazungumzia mijadala “isiyo ya moja kwa moja”

Rais wa Marekani ametoa tangazo hili wakati akimpokea Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu katika Ikulu ya White House, ambaye aliondoka bila punguzo la ushuru wa forodha uliowekewa nchi yake na Marekani wakati alikuwa amekuja kufanya mazungumzo kuhusiana na suala hilo.

Kufuatia tangazo la Donald Trump, Tehran imethibitisha msimamo wake. “Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja ya ngazi ya juu” yatafanyika nchini Oman Jumamosi, Aprili 12, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ametangaza. “Hii ni fursa kubwa kuliko mtihani.” “Mpira uko kwenye uwanja wa Marekani,” ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X. Wakati huo huo, Iran inapaswa kufanya mashauriano kuhusu suala hilo huko Moscow leo Jumanne, Aprili 8, na washirika wake wa karibu, Urusi na China.

Akiwa na msimamo mkali dhidi ya Tehran, Benjamin Netanyahu ametoa wito kutoka Washington kwa Iran “kutothubutu” kuzalisha silaha za nyuklia, akisema kuwa mazungumzo ya kidiplomasia  “yatavunjika” kabisa, akitoa mfano wa Libya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *