
Wakati Donald Trump anataka kuwahamisha Wagaza kwenda Jordan na Misri kama sehemu ya mpango wake kwa Ukanda wa Gaza, Amman na Cairo hawataki kusikia kauli hiyo. Akiwa na matumaini ya kuwalazimisha kukubali, rais wa Marekani ametangaza Jumatatu, Februari 10, kwamba “pengine” atasitiisha misaada inayotolewa kwao na Marekani ikiwa nchi hizo mbili zitaendelea kukataa kuwapoke Wapalestina kutoka Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Donald Trump ameongeza shinikizo kwa Amman na Cairo. Wakati katika mahojiano yaliyorushwa hewani jioni ya Jumatatu, Februari 10 kwenye Fox News, Donald trump amethibitisha tena nia yake ya kutwaa “milki” ya Ukanda wa Gaza, pia ameeleza kwa vyombo vya habari kwamba “pengine” atasitisha misaada inayotolewa na Marekani kwa Misri na Jordan ikiwa nchi hizi mbili zitakataa kuwapokea Wapalestina ambao wanaishi katika eneo hilo kwa sasa, sehemu ambayo rais wa Marekani hawezi kufikiria uwezekano wa wao kurudi nyumbani kwao katika mpango anaoandaa kwa Gaza.
Alipoulizwa na mwandishi a habari wa Fox News Bret Baier kama Wapalestina watakuwa na “haki ya kurejea” kwenye eneo hilo, Doald trump alijibu kwa ufanisi: “Hapana, hawataweza kurudi kwa sababu watakuwa na makazi bora zaidi.” “Kwa maneno mengine, nazungumza juu ya kuwajengea mahali pa kudumu kwa sababu ikibidi warudi sasa, itachukuwa miaka kadhaa kabla ya kufanya hivyo – haiwezekani,” ameongeza. Katika mahojiano haya, rais wa Marekani pia anaeleza kuwa Marekani inataka kujenga “jumii nzuri” kwa takriban wakazi milioni mbili wa Gaza. “Kunaweza kuwa tano, sita au mbili. Lakini tutajenga jumii salama, mbali kidogo na ambapo walipo, ambapo hatari hii yote iko,” Donald Trump ameongeza.
Mfalme wa Jordan mjini Washington siku ya Jumanne
Hata hivyo, kwa kuwa aliibua wazo la kutekeleza miradi mikubwa ya mali isiyohamishika huko Gaza, Misri na Jordan zimekataa “maelewano yoyote” ambayo yatadhoofisha haki za Wapalestina wanaoishi Gaza. Haya ni, kwa mfano, maneno ya mkuu wa diplomasia ya Misri, Badr Abdelatty, baada ya mkutano na mwenzake wa Marekani, Marco Rubio, siku ya Jumatatu mjini Washington.
Mataifa ya Kiarabu yanaunga mkono Wapalestina wanaokataa mpango wa Donald Trump wa kuchukua udhibiti wa Ukanda wa Gaza na kuwaondoa wakazi wake, alisema, kulingana na taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, ambayo ilisema pia alisisitiza kwa Marco Rubio haja ya kujenga upya eneo la Palestina na kuwaweka Wagaza katika eneo hilo.
Mfalme wa Jordan Abdullah II, ambaye nchi yake tayari inawahifadhi takriban wakimbizi milioni 2.3 wa Kipalestina, anatarajiwa kukutana na Donald Trump siku ya Jumanne, Februari 11, huko Washington. Lakini tayari wiki iliyopita, wakati bilionea huyo alipofichua mpango wake wa Gaza, pia Mfalme wa Joradan alikataa “jaribio lolote” la kuchukua udhibiti wa Maeneo ya Palestina na kuwaondoa wakaazi wao.