
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku yaJumamosi, Machi 15, kwamba jeshi la Marekani lilifanya mashambulizi dhidi ya Houthis nchini Yemen wakati wa mchana, ili kukabiliana na mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya meli katika Bahari ya Shamu. Pia ametoa wito kwa Iran “ikomeshe mara moja” msaada wake “kwa magaidi wa Houthi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 3
Matangazo ya kibiashara
” Mashambulizi haya ya Marekani “hayatasalia hivyo bila kujibiwa,” Houthi wameonya, huku mashambulizi haya yakiripotiwa kuua takriban watu 31. Leo Jumapili asubuhi, Machi 16, 2025, Tehran imejibu, na kuhakikisha kwamba Marekani “haina haki” ya kulazimisha sera yake ya nje.
Marekani “haina haki ya kulazimisha” sera ya kigeni ya Iran, mwanadiplomasia mkuu wa Iran amesema siku ya Jumapili, Machi 16, kufuatia ujumbe wa Rais Trump wa Marekani akiiamuru Iran “mara moja” kuacha uungaji mkono wake kwa Houthi nchini Yemen. “Serikali ya Marekani haina mamlaka au haki ya kulazimisha sera ya kigeni ya Iran,” Abbas Araghchi ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X, akitoa wito wa “komesha mauaji ya watu wa Yemen.”
Trump kwa Houthis: “Mtakiona cha mtema kuni”
Katika ujumbe kwenye mtandao wake wa Truth Social siku ya Jumamosi, Donald Trump ameonya kwamba ikiwa mashambulizi ya Houthi hayatakoma, “mtakipata cha mtema kuni.”
“Leo, nimeagiza jeshi la Marekani kuzindua hatua madhubuti za kijeshi dhidi ya magaidi wa Houthi huko Yemen. “Wameendesha kampeni isiyokoma ya uharamia, vurugu na ugaidi dhidi ya meli za Marekani na nyingine, ndege na ndege zisizo na rubani,” rais wa Marekani ameandika kwenye mtandao wake wa Truth Social.
“Wapiganaji wetu jasiri kwa sasa wanafanya mashambulizi ya anga dhidi ya vituo vya magaidi, viongozi, na ulinzi wa makombora ili kulinda mali ya baharini, anga na majini ya Marekani na kurejesha uhuru wa urambazaji. “Hakuna jeshi la kigaidi litakalozuia meli za kibiashara na za majini za Marekani kusafiri kwa uhuru kwenye njia za majini duniani,” Donald Trump amesema.
“Tutatumia nguvu nyingi za kuua hadi tufikie lengo letu,” rais wa Marekani ameongeza.
Trump anatoa wito kwa Iran ‘kukomesha mara moja’ kuwaunga mkono Wahouthi
“Kwa Iran: Msaada kwa magaidi wa Houthi lazima ukomeshwe mara moja!” MSIWATISHIE watu wa Marekani, Rais wao, ambaye amepewa mojawapo ya mamlaka muhimu zaidi ya urais katika historia, wala njia za meli duniani. Mkifanya hivyo, mjitahadhari, kwa sababu Marekani itawajibisha kikamilifu na hatutakuwa wazuri kwa suala hilo! “, Donald Trump pia ameandika katika ujumbe wake.
Mji mkuu wa Sanaa umekumbwa na mashambulizi ya anga, wamesema wahouthi kufuatia tangazo la Donald Trump. Kulingana na waasi wa Houthi, mashambulizi haya yamesababisha vifo vya watu 31 na zaidi ya 100 kujeruhiwa, kulingana na ripoti mpya.
“Shambulio la Marekani na Uingereza limelenga eneo la makazi kaskazini mwa mji mkuu Sanaa,” linalodhibitiwa na Houthi, kituo cha waasi cha Al-Massirah kimeripoti.
“Uchokozi huu hautasali hivyo bila kujibiwa,” wanaonya Wahouthi
“Uchokozi huu hautasalia hivyo bila jibu, na vikosi vyetu vya jeshi viko tayari kujibu uhasama kwa hasama,” ofisi ya kisiasa ya waasi imesema katika taarifa iliyotangazwa kwenye televisheni ya Al-Massirah.
Marekani ilianzisha mashambulizi hayo siku chache baada ya Wahouthi kutishia kuanzisha tena mashambulizi dhidi ya meli zinazosafiri kutoka Yemen ambazo wanaamini zinahusishwa na maslahi ya Israeli iwapo Israeli haitaondoa mzingiro wake wa Ukanda wa Gaza na kuanza tena mazungumzo ya kumaliza vita. Siku ya Jumanne jioni waasi wa Houthi walitangaza kwamba walianzisha tena “marufuku ya kupita meli zote za Israeli” katika Bahari Nyekundu, Mlango wa Bahari wa Bab el-Mandeb, Ghuba ya Aden na Bahari ya Arabia.